MKOA WA PWANI WAZINDUA MSIMU MPYA WA KILIMO IKIWEMO MPUNGA 2018/2019
Mkuu Wa Mkoa Wa Pwani mhandisi Evarist Ndikilo, akizungumza jambo kabla ya kuzindua msimu mpya wa Kilimo 2018/2019 katika mashamba ya Ushirika wa CHAURU ,huko Ruvu,Bagamoyo mkoani Pwani Na Mwamvua Mwinyi,Pwani MKUU wa mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo ,amekiagiza Chama Cha Ushirika cha Wakulima wa Umwagiliaji Ruvu (CHAURU), kumnyang’anya mwekezaji wa Kichina M/S Guoming Tang ,hekari 300 kati ya 380 alizozihodhi,ili zitumiwe na wakulima msimu mpya wa kilimo. Aidha ameuagiza ushirika huo, halmashauri ya Chalinze na serikali ya wilaya ya Bagamoyo kukakikisha hekta 1,800 kati ya 3,209 zilizopo kwenye shamba hilo ,zinatumika kupandwa mikorosho ya kisasa. Ndikilo aliyatoa maagizo hayo ,wakati wa uzinduzi wa msimu mpya wa kilimo ikiwemo mpunga 2018/2019.## Alisema ,mwekezaji huyo anapaswa kubakia na eneo atakaloweza kulifanyia kazi kuliko kuchukua eneo kubwa ambalo analikodisha na kujinufaisha nalo . “Tena asisuesue ,nashukuru uong...