JESHI LAPOLISI KUUNGANA NA MSUMBIJI KUWASAKA WAHALIFU.
Mkuu wa jeshi POLISI nchini Tanzania Inspekta Simoni SIRRO |
Timothy Marko
Jeshi la polisi nchini kwakushirikiana na jeshi lapolisi nchini Msumbiji limeingia makubaliano ya kupambana na uhalifu katika maeneo ya mipakani ikiwemo wahamihaji haramu nawaojihusisha na vitendo vya ugaidi pamoja na uhalifu wa kutumia silaha .
Akizungumza na waandishi habari jijini Dar es salaam Mkuu wa jeshi hilo nchini Tanzania Inspekta Simoni Sirro amesema kuwa hatua hiyo imetokana na kuwepo kwa taarifa kwa baadhi yawahalifu waliohusika na mauaji mkoa wa pwani kata yakibiti kutoroka nakwenda msumbiji baada ya jeshi hilo kufanya msako wa wahalifu hao .
''Taarifa zinaonesha kuwa baadhi yawahalifu waliopo kibiti mkoani pwani wamekimbilia katika nchi ya msumbiji ,niwahakikikishie wale wahalifu walio kimbilia msumbiji hawapo salama unapojiingiza kwenye uhalifu wakutumia silaha dawa yake nisilaha tunachokitaka watu wamsumbiji naafrika mashariki waaishi kwa amani ''Alisema inspeta Simon Sirro.
kwa upande wake Mkuu wa jeshi lapolisi nchini Msumbiji Inspekta Bernardino Raphaeli amesema kuwa lengo lakukutana na IGP Simon Sirro nikuimarisha ulinzi mipakani nakuhakikisha mipaka baina yanchi hizo inakuwa salama .
Alisema kuwa jeshi hilo la msumbiji linataka matatizo ya uhamiaji haramu na uhalifu katika mipaka ya nchi hizo inakuwa salama .
''tuna taka kukomesha vitendo hivi vya kiahalifu na matatizo ya uhamiaji haramu vinakomeshwa nakuhakikisha mipakayetu inakuwa salama ''Alisema inspekta Raphaeli.
Comments
Post a Comment