TBF IMEZITAKA TAASISI ZA MPIRA WAKIKAPU KUSAJILIWA .

Tokeo la picha la rais wa mpira wa kikapu

Timothy Marko
SHIRIKISHO la mpira wa kikapu nchini (TBF) imewataka wadau nawanamichezo na Taasisi mbalimbali za serikali nabinafsi zinazo shiriki mashindano ya mpira wakikapu kuweza kusajiliwa  ilikuondokana natatizo lakucheza mchezo huo chini ya kiwango nakushindwa katika ngazi za kimataifa za mashindano ya mpira huo .

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Rais wa shirikisho hilo Phares Magesa amesema kuwa kumekuwa na baadhi ya Taasisi za serikali nazile za binafsi zimekuwa zikishiriki mashindano yampira wa kikapu pasipo kuzingatia suala latakwimu za wachezaji wanao shiriki mchezo huo wenye umaarufu duniani .

''Lengo lakusajiliwa kwa taasisi za umma na zile za binafsi zinazo shiriki ni kuweza kufanya tahimini za viwango vya wachezaji wampira wakikapu pamoja na maendeleo yampira wakikapu nchini ''Alisema Rais wa Shirikisho Phares Magesa .

Rais wa TBF Magesa alisema kuwa shirikisho hilo limeweka mpango mkakati wa kubadili katiba wa maendeleo yampira wakikapu nchini ilikuweza kuendana na matakwa ya mpira huo unaosifika duniani ambapo shirikisho hilo limeweka mpango mkakati wakuunganisha vyama vyampira huo vya kutoka zanzibar kuwa shirikisho moja la mpira huo .

Alisema Tayari shirikisho hilo limesha wateua wajumbe wapatao watano ikwemo watalamu wa tiba sambamba na kamishina wanawake atayejihusha na maendeleo yamchezo huo kwa ngazi za vilabu ilikuweza kushiriki mashindano ya kimataifa .

Comments

Popular posts from this blog

Mvua yatatiza mpambano kati ya Simba SC na El Masri

Marubani Wawili Wapoteza Maisha kwa Ajali ya Ndege Zanzibar

Huduma za serikali ya Marekani zakwama kwa mara nyengine