Watoto waliofungwa minyororo wapatikana kwenye nyumba California

matwa huko California baada ya polisi kupata watu 13 waliokuwa wameshikiliwa mateka nyumbani kwao wakiwemo wengine waliofungiwa kwenye vitanda vyao kwa minyororo na makufuli.
David Allen Turpin, 57, na Louise Anna Turpin, 49, walikamatwa kwa tuhuma za mateso na kuhatarisha maisha ya watoto.
Watu hao 13 walio na umri wa kati ya miaka miwili na 29, walipatikana kwenye nyumba eneo la Perris kilomita 95 kusini mashariki mwa Los Angeles.
Wote hao wanaaminika kuwa ndugu.
Maafisa waligundua hilo siku ya Jumapili wakati mmoja wa watoto hao alifanikiwa kuponyokana na kupiga namba ya dharura akitumia simu ambayo alipata ndani ya nyumba.
Msichana huyo ambaye polisi wanasema alionekana kuwa na umri wa miaka 10, alidai kuwa ndugu zake wengine 12 walikuwa wakishikiliwa na wazazi wao
Comments
Post a Comment