ODINGA :HATUA YA LEO NI KUELEKEA UDIKITETA KUELEKEA DEMOKRASIA.


Tarehe 8 Agosti, Raila Odinda alipiga kura katika kituo cha kupiga kura katika shule ya msingi ya Old-Kibera.Raila aondoka uwanja wa Uhuru Park

Punde tu alipofika na 'kula kiapo' Raila Odinga ameondoka.
Wengi wamekuwa wakisubiri kwa hamu na ghamu, bila kutegemea kwamba atachukua muda mfupi hivyo.
Awali Raila Odinga aliiambia kituo cha habari cha KTN kwamba shughuli hio ' si mapinduzi ya serikali'

Odinga akula kiapo uwanja wa Uhuru Park

Raila Odinga amefika katika pamoja na viongozi kadha wakuu wa NASA na kujiapisha akishika Biblia.
Amewaambia kuwa mgombea mwenza wake Kalonzo Musyoka wa chama cha Wiper ataapishwa baadaye.
Viongozi wengine wenza wa Nasa Moses Wetangula na Musalia Mudavadi pia hawakufika katika wuanja huo.
Bw Odinga amesema leo ni siku ya kihistoria kwa Kenya.
"Hatua ya leo ni kuelekea kutoa udikteta na kuleta demokrasia Kenya"

Comments

Popular posts from this blog

Mvua yatatiza mpambano kati ya Simba SC na El Masri

Marubani Wawili Wapoteza Maisha kwa Ajali ya Ndege Zanzibar

Huduma za serikali ya Marekani zakwama kwa mara nyengine