WAZIRI UMMY:UJAUZITO SIO UGONJWA WANANCHI CHANGIENI HUDUMA.
![]() |
Waziri wa Afya maendeleo yajamii jinsia wazee na watoto Ummy Mwalimu |
Serikali imewatakawananchi kuweza kuchangia gharama za kujifungua pindi wanawake wanapokwenda katika hospitali za umma nakusisitiza kuwa nivyema wananchi hao wakawekeza fedha kidogo kidogo mbaka wakati wakujifungua ili kuondoa gharama za matibabu za huduma hiyo kwa serikali .
Akizungumza katika ziara hospitali ya Mkoa wa Dar es salaam ya Amana jijini hapa Waziri wa Afya maendeleo yajamii jinsia wazee na watoto Ummy Mwalimu aliwataka wajawazito kuweza kuwekeza kidogo kidogo fedha kwajili ya gharama za kujifungua na badala yake kuishushia mzigo serikali ilikuweza kutoa hudumahiyo .
''Jamani kinamama mnapaswa kuwekeza kidogo kidogo leo umepata shilingi elfu kumi kesho elfu ishirini tayari umeshapata huduma ya kujifungulia baadala kuitegemea serikali iweze kuwasaidia nilazima nanyinyi kama wakinamama muweze kuchangia huduma ''Alisema Waziri Ummy Mwalimu .
Waziri ummy alisema kuwa kupata ujauzito sio ugonjwa mbaka serikali ianze kuingia gharama yakutuoa huduma hiyo ,alisitiza kuwa nivyema wajawazito kuelewa kuwa kupata ujauzito sio ugonjwa .
Alisema serikali imewataka wauza dawa za binadamu katika hospitali za umma kuhakikisha zina nembo yaserikali ilikuweza kuondokana nawatumishi wasio waaminifu .
Comments
Post a Comment