Posts

Showing posts from September, 2017

Makamu wa Rais wa Itel Mobile Bw.Leslie Ding akizungumza na wadau pamoja na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kuanzimisha maadhimisho ya Miaka 10 ya Kampuni hiyo.

Image
Makamu wa Rais wa Itel Mobile Bw.Leslie Ding akizungumza na wadau pamoja na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kuanzimisha maadhimisho ya Miaka 10 ya Kampuni hiyo.

TAMBWE, KESSY WAREJEA LAKINI HAWANA NAFASI KESHO VS MTIBWA

Image
Mshambuliaji hatari zaidi anapoona nyavu, Amissi Tambwe ameanza mazoezi na Kocha George Lwandamina ana nafasi ya kuongeza upana wa kikosi chake. Tambwe ameanza mazoezi jana katika Uwanja wa Uhuru baada ya kuwa amefanya mazoezi ya pekee kujiandaa na kuungana na wenzake. Pamoja na Tambwe, beki wa pembeni wa Yanga, Hassan Kessy ambaye alikuwa anasumbuliwa na majeraha baada ya kupata ajali ya bodaboda, naye ameanza mazoezi akionyesha yuko vizuri tofauti na awali. Daktari wa Yanga, Edward Bavu amethibitisha wawili hao kuanza mazoezi ingawa jana walikuwa wakikimbia pembeni ili kuhakikisha wanakuwa vizuri zaidi na uhakika, watakaa nje Yanga ikiivaa Mtibwa Sugar, kesho. "Tambwe mwenye majeraha ya goti na Kessy yeye majeraha ya ajali ya bodaboda wote wapo fiti na leo (jana) waliendelea kufanya mazoezi yao ya binafsi kwa ajili ya kujiweka fiti ambao wataukosa mchezo wa keshokutwa Jumamosi dhidi ya Mtibwa kwa kuhofia kujitonesha licha ya kuanza mazoezi," alisema Bavu...

Watu kumi na wawili wameuawa na wengine zaidi ya 30 kujeruhiwa, kufuatia kisa cha mkanyagano baada ya daraja moja kuporomoka karibu na kituo cha treni, mjini Mumbai India.

Image
MTANDAO WA BBC Waliyoshuhudia wanasema, daraja hilo huenda liliporomoka kutokana mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha wakati huo, hali ambayo iliwafanya watu kukimbilia mahala hapo kujikinga. Mwandishi wa BBC mjini Mumbai, anasema mamlaka imekuwa ikilaumiwa kwa kutelekeza miundo mbinu katika mji huo licha ya kuwa mji huo unapokea watu wengi kila siku. Watu waliojeruhiwa wamefikishwa katika hospitali iliyo karibu na maafisa wakuu wa reli wapo katika eneo la mkasa. Msemaji wa shirika la reli Anil Saxena ameambia waandishi habari kuwa daraja hilo lililofunikwa lilikuwana shughuli nyingi kwasababu idadi kubwa ya wasafiri waliokuwa wanajikinga na mvua kubwa walijaribu kuondoka kwa wakatimmoja na abiria wengine. Ameongeza kuwa mkasa huo utachunguzwa.

JIJI LADAR ES SALAAM LAINGIA MAKUBALIANO NA CHINA

Image
Meya wa jiji la DAR ES SALAAM  Isaya Mwita Akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani leo  Timothy Marko  KATIKA kuhakikisha jiji la Dar es salaam linakuwa jiji la kimataifa linalohamasisha utalii wa ndani na nje jiji hilo limeingia makubaliano namakampuni yakutoka nchini china ilikuweza kuboresha miundombinu ikiwemo barabara zajuu katika wilaya ya ubungo . Akizungumza Katika makubaliano hayo jijini Dar es salaam Meya wa jiji hilo Isaya Mwita amesema kuwa jiji hilo linavutiwa nawawekezaji wakutoka nchini china kuja kuwekeza katika miradi mbalimbali ikiwemo miradi ya bandari na upanuzi wa bandari yakurasini pamoja namradi yabarabara za juu katika wilaya ubungo . ''Leo tumepata ujumbe kutoka china wa baadhi ya makampuni yajenzi namakampuni mbalimali kutoka nchini china kutaka kuwekeza katikasekta yamiundombinu ilikufanya jiji la Dar es salam kuwa jiji lakimataifa ''Alisema Meya wajiji Isaya mwita    Kwa upandewake muwakilishi wa ujumbe ...

WAFANYABIASHARA SOKO LA ILALA MCHIKICHINI JIJINI DAR ES SALAAM WAPEWA ELIMU YA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA

Image
Mwezeshaji wa kisheria kutoka Shirika la Equality for Growth  (EfG) , Amina Mussa akitoa elimu ya kupinga vitendo vya ukatili wa jinsia kwa wafanyabiashara wa Soko la Ilala Mchikichini Dar es Salaam leo. Mfanyabiashara Shikei Ngosi, akielezea changamoto zinazotokana na ukatili wa kijinsia katika soko hilo. Mwezeshaji Khadija Mohamed akitoa elimu ya upingaji wa ukatili wa kijinsia. Mfanyabiashara, Mussa Ibrahim, akichangia jambo. Juma Mohamed akichangia jambo . Mfanyabiashara wa nguo katika soko hilo, Godrey Milonge akielezea changamoto za ukati wa kijinsia katika soko hilo. Mwezeshaji wa Sheria kutoka Soko la Temeke Stereo, Batuli Mkumbukwa akichangia jambo. Mwezeshaji Sheria, wa Soko la Kigogo Kisambusa, Mariam Rashid akitoa mafunzo Mwezeshaji wa Sheria katika Soko la Ilala Mchikichini, Consolata Cleophas akitoa elimu hiyo. Mfanyabiashara, Johnson Stephano akisoma moja ya kijarida kinachoelezea ukatili huo. Mafunzo yakiendelea. Ofi...

MSUVA KUJIUNGA NA TAIFA STARS JUMATATU KWA MECHI NA MALAWI

Image
Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM WINGA Simon Happygod Msuva anatarajiwa kuwasili nchini Jumatatu kujiunga na kikosi cha timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kwa ajili ya mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Malawi wiki ijayo.   Taifa Stars itamenyana na Malawi Jumamosi ya wiki ijayo na kocha Salum Shaaban Mayanga amewaita washambuliaji wake wawili tegemeo wanaocheza nje, Msuva wa Difaa Hassan El - Jadida ya Morocco na Mbwana Ally Samatta wa KRC Genk ya Ubelgiji.   Akizungumza na Bin Zubeiry Sports – Online leo, Msuva amesema kwamba anatarajiwa kuwasili Dar es Salaam Oktoba 2, zikiwa ni siku tano kabla ya mchezo huo wa kirafiki wa kimataifa utakaofanyika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. Simon Msuva anatarajiwa kuwasili nchini Jumatatu kujiunga na Taifa Stars kwa ajili ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Malawi   “Ninashukuru nimeitwa tena timu ya taifa na tayari klabu yangu hapa imepata taarifa na nimeruhusiwa kuja nyumbani, ninatar...

NIGERIA KUWASILI KESHO KUIVAA TWIGA STARS

Image
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM TIMU ya soka ya taifa ya wanawake wenye umri wa chini ya miaka 20 ya Nigeria ‘Falconets’ inatarajiwa kutua nchini usiku wa kumkia Ijumaa Septemba 29, mwaka huu. Wakitokea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Nnamdi Azikiwe, ulioko Abuja nchini Nigeria, Falconets watatumia ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia ikiwa ni kikosi cha watu 31 miongoni mwake wako maofisa 13 kuja Dar es Salaam, Tanzania.  Timu hiyo ya wanawake yenye wachezaji 18, watatua Dar es Salaam saa 9.40 usiku na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limewapangia kuishi katika Hoteli ya Urban Rose iliyoko katikati ya jiji la Dar es Salaam katika kipindi cha siku tatu watakazokuwa hapa jijini. Wanakuja kucheza na timu ya Taifa ya wasichana wenye umri wa chini ya miaka 20 ya Tanzania ‘Tanzanite’ kwenye mchezo wa marudiano kuwania kucheza fainali za Kombe la Dunia. Fainali za Kombe la Dunia zitafanyika Ufaransa hapo mwakani. Mchezo huo wa marudiano utafanyika Jumapili O...

HALMASHAURI ZIONGEZE MABWAWA KWA AJILI YA KILIMO CHA UMWAGILIAJI; NAIBU WAZIRI KAMWELWE.

Image
Naibu Waziri Wizara ya Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack A. Kamwelwe na Mkuu wa Mkoa wa Singida wakisoma kwa umakini taarifa ya Sekta ya maji Mkoa wa Singida wakati wa kikao na wakuu wa idara mbalimbali. Naibu Waziri Wizara ya Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack A. Kamwelwe akisikiliza taarifa ya mradi wa maji wa Ughandi kutoka kwa Mhandisi wa Maji wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida Edward Kisalu. Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Singida Patrick Girigo Kasango na Kaimu Afisa Elimu Mkoa wa Singida Eva Mosha wakimsikiliza Naibu Waziri Wizara ya Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack A. Kamwelwe. Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Singida Buhacha Baltazar Kichinda akisoma taarifa ya sekta ya Maji kwa Katibu Tawala Mkoa wa Singida Buhacha Kichinda. Naibu Waziri Wizara ya Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack A. Kamwelwe akisisitiza jambo alipokuwa akizungumza na wananchi wa kijiji cha Ughandi A halmashauri ya Wilaya ya Singida alipotem...

Hatma ya Carlo Ancelloti katika klabu ya Bayern Munich kujulikana

Image
Bayern Munich itatoa tangazo kuhusu hatma ya kocha Carlo Ancelotti baadaye siku ya Alhamisi. Bodi ya timu hiyo ilikutana baada ya kichapo cha 3-0 dhidi ya PSG siku ya Jumatano. Kocha huyo mwenye umri wa miaka 58 alichukua mahala pake Pep Guardiola mwanzo wa msimu wa 2016-17. Ancelotti aliisaidia Bayern kushinda kombe la Bundesliga , lakini klabu hiyo ikaweza kufika katika awamu ya makundi ya kombe la vilabu bingwa Ulaya. Walishindwa kufika katika fainali ya DFB baada ya kushindwa 3-2 na Borussia Dortmund. Ancelotti ameshinda kombe la vilabu bingwa mara tatu mbali na mataji ya ligi nchini Itali, Uhispania, Uingereza na Ujerumani.

Myanmar yafutilia mbali ziara ya Umoja wa mataifa Rakhine

Image
  Mtandao wa BBC Umoja wa mataifa unasema kuwa, utawala wa Burma umefutilia mbali mipango ya Umoja huo kuzuru jimbo la Rakhine nchini Myanmar. Hilo ni eneo ambalo kulishuhudiwa idadi kubwa zaidi ya watu wa jamii ndogo ya waislamu Wa- Rohingya, waliotoroka makaazi yao kuepuka mapigano. Msemaji wa Umoja wa mataifa huko Yangon, Stanislav Saling, ameiambia BBC kuwa hakuna sababu zozote ambazo zilitolewa kuhusiana na hatua ya kuwazuia maafisa wa Umoja wa mataifa kuzuru maeneo hayo. Umoja wa mataifa umekuwa ukishinikiza kuruhusiwa kulizuru jimbo hilo la Rakhine, ili kupeleleza kiini cha Warohingya hao kuhama kwa wingi kutoka maeneo hayo, kuanzia mapema mwezi uliopita . Makumi kwa maelfu ya waislamu, Wabudha na Wahindu wanaishi katika majengo ya muda katika jimbo hilo la Rakhine tangu kuanza kwa mashambulio yaliyokuwa yakitekelezwa na warohingya wenye itikadi kali. Hatua iliyosababisha Jeshi la Myanmar kuanza kuwashambulia Warohingya.

SERIKALI YAWATAKA WANAHABARI KUZINGATIA MAUDHUI

Image
KATIBU MKUU WA WIZARA YA HABARI SANAA NA UTAMADUNI NA MICHEZO PROFESA ELISANTE OLEGabriel Timothy Marko. SERIKALI imewataka waandishi wa habari za mitandao kuweza kuandika habari zinazozingata maadili ya kitanzania nabadala yake kutumia mitandao hiyo kuleta habari za uchochezi ilikuondokana na matatizo ya hali ya kiusalama na mikangnyiko itakayoleta mikanganyiko ndani ya jamii. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam katika mkutano wa wadau mbalimbali wa tasinia ya Habari Katibu mkuu wa wizara ya Habari Utamaduni na Michezo Profesa Elisante Ole Gabrieli amesema kuwa nimuhimu kwa wanahabari kuzingatia suala la maudhui katika habari anayoitoa ilikuepuka mikanganyiko ndani ya jamii . ''Suala lamaudhui nimuhimu sana kwa wanataluma ya habari kwani maudhui kwenye habari ndio yanayojenga jamii ama kubomoa jamii husika hivyo hata kama mpo kibishara nilazima kuzingatia suala lamahudhui katika vyombo vya habari suala lakuonyana onyana kila siku sio suala zuri ...

OFISI YA TAKWIMU NCHINI YAPOKEA MSAADA WA TABLETS 500 KUTOKA BENKI YA DUNIA

Image
MKURUGENZI MKUU WA OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU (NBS) DK. ALBINA CHUWA AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI (HAWAPO PICHAANI) JIJINI DAR ES sALAAM LEO. Timothy Marko. OFISI ya taifa ya Takwimu nchini (NBS) imepokea msaada wa Tablets 500 kutoka Benki ya Dunia (WB)  zitakazotumika katika utafiti wa mapato na matumizi ya Kaya binafsi Tanzania bara. Msaada huo umetolewa leo umetolewa na Mkurugenzi wa benki hiyo Bi Bella Bird kwa Mkurugenzi Mkuu wa ofisi hiyo, Dk.Albina Chuwa. Akizungumza na wanahabari jijiini Dar es Salaam Mkurugenzi huyo amesema tablets hizo zitatumika kwa ajili ya zoezi la ukusanyaji wa takwimu katika utafiti wa kaya hizo katika mikoa hiyo yote kuanzia mwezi Novemba mwaka huu. " Tablets hizi zitasaidia kupunguza gharama ambazo zingetumika kuchapisha nakala za madodoso yanayotumika katika tafiti mbalimbali  zinazofanywa na ofisi ya takwimu, utaafiti huu utahusisha maeneo wakilishi 796 na kaya wakilishi 9,552 ambazo zilichaguliwa kitaalamu ili kuweza kuba...

AZAM YAIKAMATA MTIBWA KILELENI

Image
TIMU ya Azam FC, imeendelea kufanya kweli kwenye Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, baada ya kuichapa Lipuli bao 1-0, mchezo uliofanyika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam usiku wa Jumapili. Kwa ushindi huo Azam FC imefanikiwa kuikamata Mtibwa Sugar baada ya kufikisha jumla ya pointi 10 zikiwa zinalingana kileleni huku ikiwa timu pekee ambayo haijaruhusu bao lolote tokea ligi hiyo ilipoanza Agosti 26 mwaka huu. Bao pekee la Azam FC limefungwa na Mbaraka Yussuf dakika ya 11 akipokea pasi safi ya Nahodha Himid Mao ‘Ninja’, likiwa ni bao lake la pili kwenye mechi ya pili mfululizo lingine akiitungua timu yake ya zamani Kagera Sugar katika ushindi wa 1-0 Licha ya kufunga bao hilo, Azam FC ilifanikiwa kutawala mchezo huo kwa kiasi kikubwa na kutengeneza nafasi nyingi takribani 10 ambazo hazikutumiwa vema. Lakini safu ya ushambuliaji ilikuwa ikiundwa na wachezaji vijana Yahya Zayd na Yusuph, ambao wanaendelea kujifunza mikikimikiki ya ligi hiyo, Kabla ya mchezo huo, Rais wa ...

Kurdistan yapiga kura ya uhuru Iraq

Image
Sambaza habari hii Emai   Mshirikishe mwenzako Haki miliki ya picha GETTY IMAGES Image caption Wafuasi huko Irbil walikusanyika kwa idadi kubwa Ijumaa MTANDAO WA BBC Watu wa jimbo la Kurdistan nchini Iraq, wanashiriki kura ya maoni kuhusu uhuru wa eneo hilo licha ya pingamizi kutoka Baghdad, mataifa jirani na jamii ya kimataifa. Wengi wanahofia kura hiyo itachochea upya vurugu katika taifa hilo ambalo linakabiliwa na changamoto za kiusalama kutoka kwa makundi ya itikadi kali. Kiongozi wa jimbo hilo Masoud Barzani,anasema uhuru wa eneo hilo ndio njia pekee ya kuwahakikishia usalama wakurdi. Bwana Barzani ameongeza kuwa hatua hiyo haitaweka mpaka kati ya eneo hilo na Iraq na kwamba mazungumzo na Baghadad yataendelea kwa muda wa mwaka mmoja hadi miwili. Kuna hofu kura hiyo ya maoni huenda ikasambaratisha Iraq na kuchochea upya mzozo kati yake na eneo hilo ambalo linasemakana halijapata uthabiti wa kisiasa. Jamii ya kimataifa inahoji kuwa kura ya maoni inayoandaliwa l...

MAUZO YA HISA JIJINI YAFIKIA BILIONI 53.5

Image
Timothy Marko.  KIWANGO cha mauzo  ya hisa katika soko la hisa la Dar es salaam (DSE)kimeongezeka kutoka shilingi bilioni 5.4 wiki iliyopita hadi kufikia shilingi bilioni 53.5 mnamo September 22 mwaka huu . AFISA MWANDAMIZI WA SOKO LA HISA DSE MARY KINABO AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI LEO JIJINI DAR ES SALAAM Kuongezeka kwa mauzo ya hisa hizo kumetokana na kuongezeka kwa ukubwa wa mtaji katika kampuni ya Kenya Airways kwa asilimia 20 pamoja na uchumi super market kwa asilimia 12.5pamoja benki ya kibiashara ya Kenya kuongezeka kwa asilimia 9. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Afisa mwandamizi wa Soko la hisa soko hilo jijini dar es salaam Mary kinabo amesema kuwa ukubwa wamtaji wa kampuni zandani umeongezeka kutoka shilingi milioni 27 hadi kufikia shilingi trioni 9.5 ‘’Makapuni yaliyo ongoza wiki hii katika mauzo ya hisa nipamoja na Benki ya biashara ya CRDB ,DCB Pamoja na Soko lahisa la Dar es salaam’’Alisema Mary kinabo Afis...

Korea Kaskazini yafyatua kombora kupitia anga ya Japan

Image
Rais Moon Jae-in alifanya kikao cha dharura na kuonya kwamba kombora hilo litasababisha vikwazo zaidi dhidi ya Korea kaskazini. Mtandao Wa BBC Jeshi la Korea Kusini limesema kuwa jaribio hilo la hivi karibuni, likiwa la kwanza tangu vikwazo dhidi ya Korea kaskazini kuimarishwa wiki iliopita lilifanyika katika eneo la Sunan Kaskazini mwa Pyongyang. Na kama kombora la hapo awali, hili la sasa pia lilipitia katika anga ya kisiwa cha Japan kilichopo kaskazini mwa taifa hilo cha Hokkaido na kuanguka katika bahari ya pacific. Ving'ora vililia katika eneo hilo vikitoa tahadhari kwa raia kujificha. Mwanamke maarufu zaidi Korea Kaskazini Mwanafunzi anayetaka ukasomee Korea Kaskazini Mzozo wa Korea Kaskazini na Marekani kwa muhtasari Kulingana na makadirio ya awali, kombora hilo lilirushwa juu zaidi ya lile lililorushwa mnamo Agosti tarehe 29 ambalo Pyongyang ilionya ni operesheni yake ya kwanza ya kijeshi katika eneo la Pacific. Waangalizi wanasema kuwa kombora hilo ni l...

TIMU YA WANAWAKE U20 ‘THE TANZANITE’ YAIFUATA NIGERIA KUTAFUTA SAFARI YA UFARANSA

Image
Timu ya Taifa ya Tanzania ya wanasichana wenye umri wa chini ya miaka 20 ‘The Tanzanite’ imeondoka usiku  wa kuamkia leo Alhamisi kwenda Nigeria kwa Ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia. Timu hiyo inakwenda Nigeria kucheza na wenyeji katika mchezo kuwania kufuzu kucheza fainali za Kombe la Dunia. Fainali hizo za vijana kwa wasichana, zitafanyika Ufaransa, mwakani. Mchezo utafanyika Septemba 16, mwaka huu katika Uwanja wa Samuel Ogbemudia uliko Jiji la Benin kabla ya kurudiana na Tanzania wiki mbili zijazo katika uwanja na tarehe ambayo TFF itaitangaza baadaye. Timu imeondoka na wachezaji 20 na Kocha Mkuu wa timu hiyo, Sebastian Nkoma amesema wana matumaini ya kufanya vema kwenye mchezo huo ilihali Nahodha wa timu hiyo, Wema Richard akiaminisha Watanzania kurudi na ushindi akisema: “Hapa ni kazi kazi.” Timu hiyo iliagwa kwa kupewa Bendera ya Taifa jana Jumatano Septemba 13, mwaka huu na Mkurugenzi wa Michezo, Yussuph Singo na Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, Kidao Wi...

Benki ya NBC Yazindua Klabu ya Biashara Mkoani Mbeya

Image
Alex   2 days ago BIASHARA Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, William Ntinika (kushoto), akionyesha nembo mpya ya Klabu ya Biashara ya NBC mara baada ya uzinduzi rasmi wa klabu hiyo mjini Mbeya hivi karibuni. Hafla hiyo ilihudhuriwa na wateja wa NBC, wajasiriamali na maofisa waandamizi wa serikali mkoani humo. Wanaoangalia nyuma yake ni Ezekiel Mwakibinga, Mkurugenzi wa Biashara wa NBC, Elvis Ndunguru na Essau Kamwela. Mwakilishi kutoka Mamlaka ya Mapato  Tanzania (TRA), Gabriel Mwangosi (kulia), akifundisha masuala mbalimbali kuhusu kodi katika semina ya siku moja iliyoandaliwa na NBC kwa wateja wake wadogo na wa kati mjini Mbeya. Semina hiyo ilifuatiwa na uzinduzi wa Klabu ya Biashara ya benki hiyo mkoani Mbeya hivi karibuni. Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, William Ntinika (kushoto), akikaribishwa na Mkurugenzi wa Biashara wa NBC, Alvis Ndunguru wakati akiwasili kwa ajili ya uzinduzi wa  Klabu ya Biashara ya NBC mkoani Mbeya. Katikati ni Meneja Mahusiano wa NBC, Willi...