Hatma ya Carlo Ancelloti katika klabu ya Bayern Munich kujulikana

Carlo AncelottiBayern Munich itatoa tangazo kuhusu hatma ya kocha Carlo Ancelotti baadaye siku ya Alhamisi.
Bodi ya timu hiyo ilikutana baada ya kichapo cha 3-0 dhidi ya PSG siku ya Jumatano.
Kocha huyo mwenye umri wa miaka 58 alichukua mahala pake Pep Guardiola mwanzo wa msimu wa 2016-17.
Ancelotti aliisaidia Bayern kushinda kombe la Bundesliga , lakini klabu hiyo ikaweza kufika katika awamu ya makundi ya kombe la vilabu bingwa Ulaya.
Walishindwa kufika katika fainali ya DFB baada ya kushindwa 3-2 na Borussia Dortmund.
Ancelotti ameshinda kombe la vilabu bingwa mara tatu mbali na mataji ya ligi nchini Itali, Uhispania, Uingereza na Ujerumani.

Comments

Popular posts from this blog

Mvua yatatiza mpambano kati ya Simba SC na El Masri

Marubani Wawili Wapoteza Maisha kwa Ajali ya Ndege Zanzibar

Huduma za serikali ya Marekani zakwama kwa mara nyengine