Watu kumi na wawili wameuawa na wengine zaidi ya 30 kujeruhiwa, kufuatia kisa cha mkanyagano baada ya daraja moja kuporomoka karibu na kituo cha treni, mjini Mumbai India.

MTANDAO WA BBC
Waliyoshuhudia wanasema, daraja hilo huenda liliporomoka kutokana mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha wakati huo, hali ambayo iliwafanya watu kukimbilia mahala hapo kujikinga.
Mwandishi wa BBC mjini Mumbai, anasema mamlaka imekuwa ikilaumiwa kwa kutelekeza miundo mbinu katika mji huo licha ya kuwa mji huo unapokea watu wengi kila siku.Barabara ya Elphinstone inaunganisha njia mbili za reli Mumbai
Watu waliojeruhiwa wamefikishwa katika hospitali iliyo karibu na maafisa wakuu wa reli wapo katika eneo la mkasa.
Msemaji wa shirika la reli Anil Saxena ameambia waandishi habari kuwa daraja hilo lililofunikwa lilikuwana shughuli nyingi kwasababu idadi kubwa ya wasafiri waliokuwa wanajikinga na mvua kubwa walijaribu kuondoka kwa wakatimmoja na abiria wengine.
Ameongeza kuwa mkasa huo utachunguzwa.

Comments

Popular posts from this blog

Mvua yatatiza mpambano kati ya Simba SC na El Masri

Marubani Wawili Wapoteza Maisha kwa Ajali ya Ndege Zanzibar

Huduma za serikali ya Marekani zakwama kwa mara nyengine