Korea Kaskazini yafyatua kombora kupitia anga ya Japan

Kiongozi Kaskazini Kim Jong-un katika picha hii iliyotolewa na KCNA Pyongyang Septemba 3, 2017.Rais Moon Jae-in alifanya kikao cha dharura na kuonya kwamba kombora hilo litasababisha vikwazo zaidi dhidi ya Korea kaskazini.
Mtandao Wa BBC
Jeshi la Korea Kusini limesema kuwa jaribio hilo la hivi karibuni, likiwa la kwanza tangu vikwazo dhidi ya Korea kaskazini kuimarishwa wiki iliopita lilifanyika katika eneo la Sunan Kaskazini mwa Pyongyang.
Na kama kombora la hapo awali, hili la sasa pia lilipitia katika anga ya kisiwa cha Japan kilichopo kaskazini mwa taifa hilo cha Hokkaido na kuanguka katika bahari ya pacific.
BBC map
Ving'ora vililia katika eneo hilo vikitoa tahadhari kwa raia kujificha.
Kulingana na makadirio ya awali, kombora hilo lilirushwa juu zaidi ya lile lililorushwa mnamo Agosti tarehe 29 ambalo Pyongyang ilionya ni operesheni yake ya kwanza ya kijeshi katika eneo la Pacific.
Waangalizi wanasema kuwa kombora hilo ni la masafa ya wastani , ijapokuwa maafisa wa Japan wanasema kuwa kuna uwezekano mkubwa kwamba ni kombora la masafa marefu linaloweza kurushwa kutoka bara moja hadi jingine ICBM.

Comments

Popular posts from this blog

Mvua yatatiza mpambano kati ya Simba SC na El Masri

Marubani Wawili Wapoteza Maisha kwa Ajali ya Ndege Zanzibar

Huduma za serikali ya Marekani zakwama kwa mara nyengine