MAUZO YA HISA JIJINI YAFIKIA BILIONI 53.5
Timothy Marko.
KIWANGO cha mauzo ya hisa katika soko la hisa la Dar es salaam
(DSE)kimeongezeka kutoka shilingi bilioni 5.4 wiki iliyopita hadi kufikia
shilingi bilioni 53.5 mnamo September 22 mwaka huu .
AFISA MWANDAMIZI WA SOKO LA HISA DSE MARY KINABO AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI LEO JIJINI DAR ES SALAAM |
Kuongezeka kwa mauzo ya hisa hizo kumetokana na kuongezeka kwa ukubwa wa mtaji katika kampuni ya Kenya Airways kwa asilimia 20 pamoja na uchumi super market kwa asilimia 12.5pamoja benki ya kibiashara ya Kenya kuongezeka kwa asilimia 9.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Afisa
mwandamizi wa Soko la hisa soko hilo jijini dar es salaam Mary kinabo amesema
kuwa ukubwa wamtaji wa kampuni zandani umeongezeka kutoka shilingi milioni 27
hadi kufikia shilingi trioni 9.5
‘’Makapuni
yaliyo ongoza wiki hii katika mauzo ya hisa nipamoja na Benki ya biashara ya
CRDB ,DCB Pamoja na Soko lahisa la Dar es salaam’’Alisema Mary kinabo
Afisa
Mwandamizi wa soko la hisa Kinabo alisema kuwa wakati mauzo ya hisa ya kiongezeka kutoka bilioni 5.4hadi kufikia
shilingi trioni9.5 mauzo ya hati fungani hadi kufikia September mwaka huu
yameongezeka kutoka bilioni 22 hadi kufikia bilioni 36.
Alisema kuwa
kiashiria cha kampuni za ndani TSI kimepanda kutoka pointi 11 kutoka 3.704 hadi
pointi 3,715.
Comments
Post a Comment