OFISI YA TAKWIMU NCHINI YAPOKEA MSAADA WA TABLETS 500 KUTOKA BENKI YA DUNIA
![]() |
MKURUGENZI MKUU WA OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU (NBS) DK. ALBINA CHUWA AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI (HAWAPO PICHAANI) JIJINI DAR ES sALAAM LEO. |
Timothy Marko.
OFISI ya taifa ya Takwimu nchini (NBS) imepokea msaada wa Tablets 500 kutoka Benki ya Dunia (WB) zitakazotumika katika utafiti wa mapato na matumizi ya Kaya binafsi Tanzania bara.
Msaada huo umetolewa leo umetolewa na Mkurugenzi wa benki hiyo Bi Bella Bird kwa Mkurugenzi Mkuu wa ofisi hiyo, Dk.Albina Chuwa.
Akizungumza na wanahabari jijiini Dar es Salaam Mkurugenzi huyo amesema tablets hizo zitatumika kwa ajili ya zoezi la ukusanyaji wa takwimu katika utafiti wa kaya hizo katika mikoa hiyo yote kuanzia mwezi Novemba mwaka huu.
" Tablets hizi zitasaidia kupunguza gharama ambazo zingetumika kuchapisha nakala za madodoso yanayotumika katika tafiti mbalimbali zinazofanywa na ofisi ya takwimu, utaafiti huu utahusisha maeneo wakilishi 796 na kaya wakilishi 9,552 ambazo zilichaguliwa kitaalamu ili kuweza kubainisha viashiria vya umaskini na viashiria vingine," amesema Dk Chuwa.
Amesisistiza kuwa katika utekelezaji wa mapango wa maendeleo endelevu wa miaka mitano umegawanywa katika awamu mbili(FYDP-11) 2016/17 sambamba na Mpango waa Maendelevu Endelevu wa mwaka 2021 pamoja na mpango wa maendeleo endelevu (SDGs 2030).
Ameongeza kuwa ili kuwezesha kufaanyika kwa utafiti mbalimbali zinazohusiana na umaskini ni muhimu kwa mikoa na wilaya kushirikishwa katika utafiti huo.
Amefafanua kuwa kupata tablets hizo ni kuweza kupunguza matumizi ya karatasi naa kuendana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia huku akiwataka wadau wote kushiriki katika mchakato wa takwimu ili kujiletea maaendeleo kwani suala laa takwimu halimuachi mtu nyuma.
Comments
Post a Comment