Posts

Showing posts from June, 2018

Adebayo Akinfenwa: Sergio Ramos ana bahati hatutakutana uwanjani

Image
\MTADAO  WA BBC Mshambuliaji wa klabu ya Uingereza ya Wycombe Wanderers Adebayo Akinfenwa ametoa onyo kali kwa nahodha wa Real Madrid Sergio Ramos. Ramos amekuwa akishutubiwa baada ya nyota wa Liverpool na Misri Mohamed Salah kuumia begani walipokabiliana wakati wa fainali ya Kombe la Klabu Bingwa Ulaya. Ramos pia aligongana na kipa wa Liverpool Loris Karius na inadaiwa kwamba huenda tukio hilo lilimduwaza kwa kumsababishia mtikisiko wa ubongo jambo ambalo pengine lilichangia makosa ya kushangaza aliyoyafanya kipa huyo. Makosa yake mawili yalichangia mabao mawili ya Real Madrid ambao walishinda mechi hizo 3-1. Sergio Ramos afunguka kuhusu kuumia kwa Mo Salah Akinfenwa ameandika kwenye Twitter kwamba daima atakuwepo kuwasaidia na kuwaunga mkono Liverpool wakitishiwa. Amepakia video kwenye mtandao huo wa kijamii akionesha nguvu zake kwa kuvuta buti kwa kutumia mikono yake mwenyewe. Klabu yake inatokea High Wycombe eneo la Buckinghamshire, England na inachez...

Kenya yawakamata wavuvi 109 wa Tanzania

Image
   MTANDAO WA BBC Jeshi la wanamaji wa Kenya liliwakamata raia 109 wa Tanzania kwa kushiriki katika uvuvi haramu katika himaya ya maji ya Kenya katika bahari hindi. Wavuvi hao walikamatwa katika eneo la Shimoni , linalomiliki bandari kusini mashariki mwa Kenya karibu na mpaka na taifa la Tanzania na kuwasilishwa mbele ya mahakama ya kaunti ya Kwale siku ya Jumatatu. Wavuvi hao walizuiliwa baada ya kushindwa kulipa dhamana ya shilingi 20,000 za Kenya kila mmoja wao lilisema gazeti la Biashara nchini Kenya Business Daily , likimnukuu naibu wa kamishna wa Lungalunga Josphat Biwott. Hatahivyo serikali ya Tanzania tayari imeanza harakati za kuhakikisha kuwa raia hao wanaachiliwa huru. Naibu waziri wa uvuvi na ufugaji nchini Tanzania Abdalla Ulega ameliambia gazeti la The Citizen nchini humo kwamba juhudi zimeanza ili kuona kuwa tatizo hilo limetatuliwa. ''Tayari tumezungumza na wizara ya maswala ya kigeni na jeshi la polisi ili kuona vile tatizo hilo lit...

NGOMA NJE MIEZI MIWILI NA NUSU ZAIDI, AZAM FC KUMSAJILI NCHIMBI WA NJOMBE MJI FC

Image
Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM MSHAMBULIAJI Mzimbabwe, Donald Ngoma atakuwa nje kwa miezi miwili na nusu baada ya kujiunga na Azam FC akiendelea na matibabu ya mguu wake alioumia akiwa Yanga. Hiyo ni baada ya vipimo alivyofanyiwa nchini Afrika Kusini wiki iliyopita na kupewa matibabu na programu maalum ya mazoezi, ambavyo ataendelea navyo kwa miezi miwili na nusu kabla ya kurudi rasmi uwanjani. Azam FC ilimchukua Ngoma kwa makubaliano ya akafanyiwe vipimo ambayo vikiwa na majibu mazuri atapewa mkataba. Na habari zinasema baada ya vipimo hivyo nchini Afrika Kusini ambako aliongozana na Daktari Mkuu wa klabu, Mwanandi Mwankemwa, Azam FC imeridhika kumsajili Ngoma. Donald Ngoma atakuwa nje kwa miezi miwili na nusu baada ya kujiunga na Azam FC  Beki chipukizi wa kulia Azam FC, Abdul Omary ‘Hamahama’, ameongezewa mkataba wa miaka miwili  Ngoma na Mwankemwa wanatarajiwa kurejea mjini Dar es Salaam leo usiku na kesho atasaini mkataba wa kujiunga ras...

MFUMUKO WA BEI NCHINI WA PUNGUA

Image
Mkurugenzi wa takwimu zauchumi nawatu Epharaimu Kwesigabo TIMOTHY MARKO MFUMUKO wa bei nchini kwakipindi cha mwezi mei mwaka huu umeshuka nakufikia 3.6 ikilinganishwa na nasilimia 3.8 kwakpindi cha mwezi April mwaka jana . Kupungua kwa mfumuko wa bei  katika kipindi cha mwezi mei mwaka huu kumetokana nakupungua kwa mfumuko wa bei za bidhaa za vyakula ambapo baadhi ya bidhaa zilizopungua bei ni pamoja na Mahindi kwa asilimia 10.3 unga wa mahindi kwa asilimia 12 .5 mtama asilimia 13.8 ,unga wa muhogo kwa asilimia 15.2 wakati viazi mviringo vimepungua kwa asilimia 9.0  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa takwimu zauchumi nawatu Epharaimu Kwesigabo amesema kuwa wakati mfumuko wa bei nchini Tanzania ukipungua kwa asilimia 3.6 nchini kenya mfumuko wa bei umeongezeka kwa asilimia 3.95 kutoka 3.73  ''NCHINI uganda mfumuko wa bei umepungua kwa asilimia 1.7 kutoka asilimia 1.8 katika kipindi cha mwezi Aprilmwaka huu ''Alisema KWESI...

Rais Museveni ataka marufuku ya plastiki itekelezwe Uganda

Image
Image caption Sababu kuu ya kuidhinisha marufuku hiyo plastiki ni kusaidia kulinda mazingira. Rais Yoweri Museveni ameamrisha maafisa wa usalama nchini kuhakikisha kuwa marufuku ya kutumia mifuko ya plastiki nchini inatekelezwa. Ametaka kampuni 45 nchini za kutengeneza plastiki kusitisha utengenezaji wa mifuko ya plastiki katika hatua ya kufufua marufuku ya serikali ambayo imekuwepo lakini isiyotekelezwa. "Marufuku ya utengenezaji, usambazaji na uuzaji na matumizi haijafutiliwa mbali na inapswa kutekelezwa, alisema Museveni. Marufuku ya mifuko ya plastiki Kenya imefanikiwa? Wanasayansi wagundua viwavi wanaokula plastiki Sheria ya mwaka 2009 ya fedha inapiga marufuku "uingizaji, utengenezaji, uuzaji na utumiaji wa mifuko na magunia ya plastiki kuanzia Machi 31, mwaka 2010. Hatahivyo kama ilivyo kwa baadhi ya mataifa yalioendelea, utekelezaji wa sheria hiyo ndio tatizo, ni nchini Uganda ni kama ambaye ziligonga mwamba kufuatia tofuati zilizoibuka miongoni mwa m...

TANZANIA KUWA MWENYEJI WA CHANGAMOTO ZA MADAWATI YAKIJINSIA JUNE 13

Image
jaji kiongozi wa  Mahakama ya Tanzania Dk Eliezer  Feleshi Timothy Marko Tanzania inatarajiwa kuwa mwenyeji wa mkutano wa kujadili changamoto za madawati ya kijinsia na kutoa mapendekezo barani afrika kuanzia juni 13 mwaka huu mkoani ARUSHA . Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam jaji kiongozi wa Mahakama ya Tanzania Dk Eliezer Feleshi amesema kuwa mkutano huo unatarajiwa kuwa na wajumbe wapatao 350 wakutoka katika bara lafrika ambapo ajenda yamkutano huo inatarajiwa kuwa uzingatia wa kijinsia katika masuala ya utoaji haki na kusilikiza migogoro . ''tumesha anza kupokea wageni kutoka sehemu mbalimbali katika bara la afrika ambapo katika katiba yetu inazuia ubaguzi waaina yeyote nakuzingatia usawa wa kijinsia ambapo tanzania imekuwa mtekelezaji wa masula ya usawa wakijinsia katika utoaji haki hadi hivi sasa tunao majaji wanake na mahakimu majaji ambao ni wanawake ''Alisema Dk Eliezer FELESHI . Dk.FELESHI alisema kuwa mkutano huo utajumuisha ...

SERIKALI YAWATAKAWANANCHI KUDUMISHA USAFI WA MAZINGIRA .

Image
MAKAMU WA RAIS  SAMIA HASSAN SULUHU . Timothy Marko SERIKALI imewataka wanachi kudumisha hali yausafinakufanya usafi katika maeneo yao nakutunza vyanzo vya maji ilikuondokana uharibifu wa mazingira nchini . Wito huo umetolewa na Makamu wa Rais wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Hassani Suluhu wakati akifunga kilele cha maazimisho yawiki ya mazingira iliyofanyika katika viwanja vya mnazi moja jijini Dar es salaam ambapo amesema niwajibu wajamii kutunza vyanzo vya maji ili kuhifadhi viumbe ambao hadi hivi sasa wapo hatarini kutokana na uharibifu wa mazingira . ''inakadiriwa zaidi ya viumbe35000 wapo hatarini kutoweka duniani ,matunda yaasili nayopia yapo hatarini kutoweka kutokana nauharibifu wa mazingira ''Alisema Makamu wa Rais Samia Suluhu Makamu wa Rais Samia alisema kuwa jamii inapaswa kuachana natabia yakukatamiti ilikuondokana natatizo laukosekanaji wamatunda ya asili ambayo mengi ni dawa nakutaka jamii kuitunza miti hiyo . Alisema zao lakahawa...

SERIKALI KUWEKA MKAKATI WA KUPAMBANA NA VIWAVI JESHI KATIKA MAZAO.

Image
waziri wakilimo Dk charles chizeba  Timothy Marko. SERIKALI imesema tatizo la kushambuliwa kwa mazao nawadudu waviwavi jeshi katika baadhi yamazao yachakula nabiashara halipo Tanzania pekeyake bali tatizo hilo tayari limeshawahi kutokea katika nchi za afrika magharibi jitihada za kusambaza dawa kukabiliana natatizo hilo zina endelea . Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam waziri wakilimo Dk charles chizeba amesemakuwa kumekuwa na changamoto yakutatua sualahilo kwa baadhi ya wauzaji wa pembejeo za kilimo kuzalisha wadudu hao kitalamu nakusababisha tatizo hilo iliwaweze kunufaika kibiashara . ''Suala la viwavi jeshi halijaanziaTanzania pekeyake bali lilianzia huko amerika mdudu huyu amevuka mbaka afrika magharibi ndio akaja nchini TANZANIA ,hata nchi ya kenya tatizo hili lipo lakini kusiana dawa yakukabiliana natatizo hili zipo na zinapatikana ''Alisema Waziri wa Kilimo Dk Charles chizeba . Dk Chizeba alisema kuwa kuhusiana kusitishwa...