Adebayo Akinfenwa: Sergio Ramos ana bahati hatutakutana uwanjani

Adebayo Akinfenwa of Wycombe Wanderers standing on the pitch at Fratton Park\MTADAO  WA BBC

Mshambuliaji wa klabu ya Uingereza ya Wycombe Wanderers Adebayo Akinfenwa ametoa onyo kali kwa nahodha wa Real Madrid Sergio Ramos.

Ramos amekuwa akishutubiwa baada ya nyota wa Liverpool na Misri Mohamed Salah kuumia begani walipokabiliana wakati wa fainali ya Kombe la Klabu Bingwa Ulaya.

Ramos pia aligongana na kipa wa Liverpool Loris Karius na inadaiwa kwamba huenda tukio hilo lilimduwaza kwa kumsababishia mtikisiko wa ubongo jambo ambalo pengine lilichangia makosa ya kushangaza aliyoyafanya kipa huyo.

Makosa yake mawili yalichangia mabao mawili ya Real Madrid ambao walishinda mechi hizo 3-1.

Akinfenwa ameandika kwenye Twitter kwamba daima atakuwepo kuwasaidia na kuwaunga mkono Liverpool wakitishiwa.

Amepakia video kwenye mtandao huo wa kijamii akionesha nguvu zake kwa kuvuta buti kwa kutumia mikono yake mwenyewe.

Klabu yake inatokea High Wycombe eneo la Buckinghamshire, England na inacheza ligi ya daraja ya tatu kwa sasa.

'

Comments

Popular posts from this blog

Mvua yatatiza mpambano kati ya Simba SC na El Masri

Marubani Wawili Wapoteza Maisha kwa Ajali ya Ndege Zanzibar

Huduma za serikali ya Marekani zakwama kwa mara nyengine