Posts

Showing posts from May, 2018

HIMIDI MAO AOMBA KUONDOKA AZAM

Image
Nahodha wa Azam FC, Himid Mao ameuomba uongozi wa klabu hiyo umuachie aondoke. Hamid ameomba kwenda kucheza nje ya nchi na tayari amesema ameishapata klabu mpya. Kiungo huyo anataka kwenda kucheza nje akianza na majaribio na uongozi wa Azam FC, umekubali. Msemaji wa Azam FC, Jaffar Iddi Maganga amesema wanaona ni sahihi kumpa nafasi Himid akajaribu bahati yake.

Kodi ya mitandao ya kijamii: Raia Uganda kutozwa kodi kutumia Facebook na WhatsApp

Image
Sambaza habari hii Facebook   Sambaza habari hii Twitter   Sambaza habari hii Messenger   Sambaza habari hii Email   Mshirikishe mwenzako Image caption Bwn. Museveni alisisitiza kuwa ya kijamii inapaswa kulipa kodi kwasababu inachochea taarifa za udaku Raia wa Uganda wanaotumia mitandao ya kijamii nchini humo huenda wakalazimika kulipa ndipo waruhusiwe na serikali kutumia mitandao ya kijamii kama vile Facebook na WhatsApp. Hii ni baada ya Bunge hilo kuidhinisha mswada huo tata Jumatano. Chini ya sheria hiyo ambayo inatarajiwa kuanza kutekelezwa 1 Julai, wanaotumia mitandao ya kijamii watakuwa wanatozwa shilingi 200 za Uganda ambazo ni sawa na $0.05 ( £0.04) kila siku. Raia pia watalipia kila shughuli ya kibiashara watakayoikamilisha kupitia simu zao, huku kila shughuli ya kibiashara ikitozwa 1% ya thamani yake. Papa Francis awatahadharisha watawa kuhusu matumizi ya mitandao Ni vyema kuweka picha za mwanao mtandaoni? Rais Yoweri Museve...

SERIKALI YAWATAKA WANANCHI KUJIFUNZA NISHATI MBADALA KUKABILIANA UHARIBIFU WA MAZINGIRA .

Image
WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA . Timothy Marko KATIKA kupambana natatizo la uharibifu wa mazingira ikiwemo ukataji miti ovyo kwajili ya matumizi nishati ya mkaa wito umetolewa  naserikali kwa wananchi nchini kote kuja kutazama maonesho ya wiki yamazingira nchini yanayofanyikamnazi moja jijiniDar es salaam kuangalia nakujifunza njia mbadala ili kuweza kuondokana na tatizo hilo . Wito huo umetolewa na Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Kasimu majaliwa katika wiki yamazingira iliyoanza leo jijini hapa ambapo amezitaka taasisi zote zilizopo chini a serikali pamoja nabinafsi kuadhimisha siku ya mazingira ya umoja wa mataifa kwa vitendo . ''Ninatoa wito kwa vyuo vyote vikusanyike kufanya tathimini ya uharibifu wa mazingira ilikuweza kutatua tatizo hili napia nawataka viongozi wadini kuhamasisha waumini wao juu ya utunzaji mazingira ''alisema Waziri mkuu KASIMU MAJALIWA . Waziri mkuu MAJALIWA alisema katikamikakati iliyopo ya serikali nikujenga kingo za uk...

TWIGA BANCOP KUWA CHINI YA UANGALIZI WA BENKI KUU.

Image
Timothy Marko SERIKALI imeiweka benki ya kibishara ya Twiga Bancop chini ya uangalizi wa benki ya posta ambayo inamilikiwa na benki kuu nakutaka benki hiyo kuungana na benki ya posta nakuwa benki moja kuanzia kesho . Hatua ya serikali kuweka benki ya twiga bancop chini yauangalizi wa benki kuu imetokana na benki hiyo kuwa na upungufu mkubwa wa mtaji kinyume ya matakwa ya sheria ya mabenki na taasisi za fedha ya mwaka2006  hali iliyotokana na benki hiyo kuwa usalama mdogo wa sekta ya kifedha katika benki hiyo . Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Naibu Gavana wa benki kuu Benard Gese amesema kuwa katika kuhakikisha sekta yakibenki inaimarika serikali imeamua kuimarisha usimamizi wake dhidi ya benki hiyo kwa kuunganisha na benki yaposta ambayo pia inamilikiwa na serikali . ''Kwamujibu wakifungu cha 30 (1)a cha sheria yamabenki ya mabenki natasisi zake ya mwaka2006 benki kuu ya tanzania imeidhinisha benki yatwiga na tpb kuwa benkimoja kuanzia leo '...

Serikali yapokea Bilioni 4 kutoka Eu

Timothy Marko Katika kuhakiasha sekta ya ELIMU inaleta matokeo chanya katika ukuwaji wa uchumi wa viwanda jumuhia ya ulaya imeipa Tanzania shilingi bilioni 4ilikuwezeshavyuo mbalimbali kufanya utafiti. Akizungumza katika uzinduzi  mkutano wa kuhamasisha kufanya utafiti ili kujiletea maendeleo nchini WAZIRI wa ELIMU na mafunzo ya ufundi professa Joyce ndalichako amesema kuwa endapo taasisi za kielimu zitahamasisha wanafunzi wao kufanya utafiti kutasaidia kukuza kiwango cha ELIMU nchini. "Ziara za kimasomo Nje ya nchi kutaweza kukuza sekta yaelimu,tafiti nimuhimu katika kufikia uchumi wa kati" alisema WAZIRI profesa ndalichako. Profesa ndalichako alisema kuwa ufadhili wa masomo katika jumuhia ya ulaya kutawezesha wanafunzi wa uzamili Na uzamivu kupata uzoefu.