SERIKALI YAWATAKA WANANCHI KUJIFUNZA NISHATI MBADALA KUKABILIANA UHARIBIFU WA MAZINGIRA .
WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA . |
KATIKA kupambana natatizo la uharibifu wa mazingira ikiwemo ukataji miti ovyo kwajili ya matumizi nishati ya mkaa wito umetolewa naserikali kwa wananchi nchini kote kuja kutazama maonesho ya wiki yamazingira nchini yanayofanyikamnazi moja jijiniDar es salaam kuangalia nakujifunza njia mbadala ili kuweza kuondokana na tatizo hilo .
Wito huo umetolewa na Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Kasimu majaliwa katika wiki yamazingira iliyoanza leo jijini hapa ambapo amezitaka taasisi zote zilizopo chini a serikali pamoja nabinafsi kuadhimisha siku ya mazingira ya umoja wa mataifa kwa vitendo .
''Ninatoa wito kwa vyuo vyote vikusanyike kufanya tathimini ya uharibifu wa mazingira ilikuweza kutatua tatizo hili napia nawataka viongozi wadini kuhamasisha waumini wao juu ya utunzaji mazingira ''alisema Waziri mkuu KASIMU MAJALIWA .
Waziri mkuu MAJALIWA alisema katikamikakati iliyopo ya serikali nikujenga kingo za ukuta katika mto msimbazi ilikuweza kuzuia mafuriko katika mto msimbazi ambapo alisisitiza katika kuhamasisha utunzaji wa mazingira kutakuwa natunzo maaluum yautunzaji wa mazingira .
ALISEMA zaidi ya asilimia 90 ya watanzania wamekuwa wakitumia nishati ya mkaa nakuni wakati jiji la Dar es salaam pekeyake imekuwa ikitumia zaidi ya asilimia 70 ya nishati hiyo kwa matumizi ya nyumbani ambapo aliwahamasisha wananchi kutumia nishati ya gesi kama nishati mbadala .
''Nimatumani yetu kwenye suala la nishati yakupikia gesi yamtwara itakuwa nisuluhisho ,ningependa kupendekeza mitungi ya gesi ifungiwe mita ilikuweza kujua kiasi cha mtumiaji wa gesi ya mitungi ''Aliongeza WAZIRI MKUU MAJALIWA .
Comments
Post a Comment