DOROTHY SEMU AJITOA MBIO ZA URAIS ACT WAZALENDO, MPINA AINGIA KWA KISHINDO

 

Na Timothy Marko, Dm News - MWENYEKITI wa Chama cha ACT Wazalendo, Dorothy Semu, ametangaza rasmi kujiondoa katika kinyang’anyiro cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa niaba ya chama hicho, akisema hatua hiyo inalenga kulinda umoja na maslahi mapana ya chama.

Akizungumza mbele ya wajumbe wa Halmashauri Kuu ya chama katika kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Hakainde Hichilema, Makao Makuu ya ACT Wazalendo, Dorothy Sembu amesema kuwa amejiondoa kwenye kinyang'anyiro cha Kuwania kiti cha Urais kupitia Chama hicho kwa maslahi ya Chama cha ACT Wazalendo na Umma wa Tanzania kwaujumla.


“Kwa kutambua fursa na maslahi mapana ya chama chetu, nimeamua kuondoa fomu yangu kama Mgombea Urais, na kuacha fursa hii kwa mwanachama ambaye chama kitaona anafaa kwa wakati huu.”Amesema Mwenyekiti wa Chama cha ACT -Wazalendo Dorothy Sembu.

Uamuzi huo umekuja siku moja baada ya aliyekuwa Mbunge wa CCM, Luhaga Mpina, kujiunga rasmi na ACT Wazalendo. Mpina alipokewa na viongozi waandamizi wa chama na tayari ameomba ridhaa ya kuwa mgombea urais kupitia ACT, pamoja na mwanachama mwingine, Aaron Kalikawe.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi ya chama, Mkutano Mkuu Maalum wa ACT Wazalendo unatarajiwa kufanyika leo, ambapo wanachama watawachagua wagombea wa nafasi ya urais kwa pande zote mbili za Muungano – Tanzania Bara na Zanzibar. 

Kwa upande wa Zanzibar, chama kimemteua Othman Masoud Othman, Mwenyekiti wa chama hicho, kuwa mgombea pekee.

Hatua ya Semu kujiondoa imezua mjadala mpana miongoni mwa wanachama na wachambuzi wa siasa, huku wengi wakitafsiri hatua hiyo kama njia ya kutoa nafasi kwa sura mpya zinazojiunga na chama, wa zikiwemo zile zenye ushawishi mkubwa wa kisiasa kama Mpina.

Kadri hali ya kisiasa inavyoendelea kupamba moto kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, macho na masikio sasa yananaelekezwa kwa ACT -Wazalendo.

Comments

Popular posts from this blog

Mvua yatatiza mpambano kati ya Simba SC na El Masri

Marubani Wawili Wapoteza Maisha kwa Ajali ya Ndege Zanzibar

TANZANIA KUWA MWENYEJI WA CHANGAMOTO ZA MADAWATI YAKIJINSIA JUNE 13