WAZIRI UMMY ALIA NA VIONGOZI WADINI JUU YA SARATANI .
Waziri wa afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Ummy Mwalimu |
SERIKALI imewataka viongozi wadini kuwahamasisha wauminiwao katika nyumba mbalimbali za ibada juu uanzishwaji wa chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi itakayo wahusu wasichana wenye umri kati ya miaka 14 nakuendelea itayoendeshwa nchi nzima nakusisitiza kuwa chanjo hiyo haina madhara ya kiafya kama ilivyo kaririwa na baadhi yawatu .
Akizungumza katika kongamano lililowakutanisha viongozi wadini jijini Dar es salaam Waziri wa afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Ummy Mwalimu amewataka viongozi wadini kuwahimiza waumini wao wakiwemo wazazi na walezi kuwa himiza wasichana wenye umri kati miaka14 nakuendelea kufika katika vituo vya afya ilikuweza kupata chanjo hiyo .
''Ninawaomba viongozi wadini mtusaidie kufikisha ujumbe wa uanzishwaji wa uanzishwaji wa chanjo ya kuzuia saratani ya mlango wa kizazi kwa mabinti wa miaka 14 iliwawezekukingwa dhidi ya madhara yanayoweza kuwapata hapo ikiwemo kuugua kwa maumivu makali na hatmaye kifo ''alisema Waziri ummy mwalimu
waziri wa afya ummy mwalimu alisema kuwa inakariwa zaidi wanawake 670 hupata saratani ya mlango wa kizazi kila mwaka ambapo saratani hiyo huchangia vifo kwa wanawake ikifuatiwa na saratani ya matiti ambapo nizaidi ya 50 ya vifo vyote vya kinamama .
Comments
Post a Comment