TTCL Corporation kwa kushirikiana na tiGO Tanzania wazindua huduma ya kifedha (E-Money Joint)

Mkuu wa Kitengo cha TTCL Pesa
Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) Bw. Moses Alphonce (kulia) na
Afisa Mkuu wa Kitengo cha Huduma ya Fedha Tigo Bw. Hussein Sayed
wakipongezana kama ishara ya uzinduzi rasmi wa huduma za kifedha kwa jia
ya mtandao katika ya TTCL Pesa na Tigo Pesa hafla hiyo imefanyika
kwenye Ukumbi Golden Jubilee Tower (PSPF) jijini Dar es salaam leo.

Mkuu wa Kitengo cha TTCL Pesa
Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) Bw. Moses Alphonce (kulia) na
Afisa Mkuu wa Kitengo cha Huduma ya Fedha Tigo Bw. Hussein Sayed
wakipongezana kama ishara ya uzinduzi rasmi wa huduma za kifedha kwa jia
ya mtandao katika ya TTCL Pesa na Tigo Pesa hafla hiyo imefanyika
kwenye Ukumbi Golden Jubilee Tower (PSPF) jijini Dar es salaam leo,
kulia ni Nasra Mugheiry Meneja Huduma na Maendeleo ya Bidhaa TTCL Pesa
na kushoto ni Angelina Pesha Mkuu wa Kitengo cha Udhibiti wa Ubora Tigo
Pesa.

Mkuu wa Kitengo cha TTCL Pesa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) Bw. Moses Alphonce akizungumza katika zunduzi huo.

Afisa Mkuu wa Kitengo cha Huduma ya Fedha Tigo Bw. Hussein Sayed akizungumza katika mkutano huo.

Mkuu wa Kitengo cha TTCL Pesa
Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) Bw. Moses Alphonce (kulia) na
Afisa Mkuu wa Kitengo cha Huduma ya Fedha Tigo Bw. Hussein Sayed wakiwa
katika picha ya pamoja na wafanyakazi wenzao wa TTCL na Tigo mara baada
ya uzinduzi huo.
………………………………………………………………………………………………
Na Stahmil Mohamed
Shirika la mawasiliano Tanzania TTCL limeingia makubaliano ya ushirikiano wa biashara na kampuni ya simu za mikononi ya Tigo yatakayowezesha wateja wa taasisi zote mbili kubadilishana fedha na huduma za fedha kupitia simu zao za mkononi.

Hayo yamesemwa na mkuu wa Huduma
za TTCL pesa Bw.Moses Alphonce katika ghafla ya kutangaza ushirikiano
huo nakusema kuwa kwa kushirikiana na tigo pesa katika kuwapa wananchi
suluhisho sahihi la mahitaji yao ya kifedha ikiwa ni kuunga mkono
jitihada za serikali ya awamu ya tano za kusogeza huduma karibu zaidi na
wananchi.
Aidha Bw.Alphonce amesema TTCL
imeazimia kuwapa wananchi huduma za kiwango cha juu na cha ubora na
unafuu wa gharama za kutuma ,kupokea na kufanya miamala kwa kutumia simu
Zao hivyo wamedhamiria kubadili mifumo ya malipo yote ya umma na
binafsi yafanyike kupitia mtandao ili kuongeza usalama na ufanisi wa
shughuli za kiuchumi na kijamii.
Comments
Post a Comment