ISRELI YAINGIA MAKUBALIANO YA KIUSALAMA NA TANZANIA .

T\
Timothy Marko
KATIKA Kuhakikisha tatizo ugaidi na uharamia vinakomweshwa katika maeneo yamipaka ya bahari Serikali ya Tanzania leo imeingia makubaliano na serikali ya Israeli ilikuweza kutoa mafunzo maalumu yatakayotolewa kwa jeshi la wananchi pamoja na vyombo vya usalama ilikuweza kukabilana navitendo hivyo.
Akizungumza na waandishi wa Habari katika makao makuu ya wizara yaulinzi jijini Dar es salaam Waziri wa ulinzi najeshi lakujengataifa Dk.Husseni Mwinyi amesema kuwa serikali ya israeli imekubaliana na Tanzania katika kuendesha mafunzo maalumu yakukabiliana na vitendo vya uharamia kwa kutumia vyombo vyakisasa kama vinavyotumiwa na nchi hiyo ya Israeli.
''Tayari isreli walishwahi kufanya mafunzo nasisi lakini tunataka kuongeza ujuzi ikiwemo kubadilishana taarifa za kintegelensia hapo awali nchi yetu ilikuwa imelegalega kimahusiano yake na Isreli hii nikutokana na vita baridi lakini sasa Tanzania ipo katika nchi zisizo fungamana upande wowote ndio maana tumerudisha mahusiano yetu nanchi ya israeli''Alisema Waziri wa ulinzi najeshi lakujenga Taifa .
Waziri Mwinyi alisemakuwa uhusiano wa isreli niwakihistoria ikumbukwe nchi ya israeli ndio nchi yakwanza kuwa najeshi lakujenga taifa ambapo mfumuo huo huo umeweza kujenga jeshi lakujenga Taifa nchini Tanzania
Alisema tayari nchi ya TANZANIA imeshafungua ubalozi wake katika nchi hiyo mjini telaviv hii inamanishakuwa nchi ya tanzania haifungamani na upande wowote .
KATIKA hatua nyingine Waziri waulinzi wa israeli Avigdor LIBERAMAN amesema kuwanchi yake imelenga kutoa mafunzo yakusalama kwa masuala mbalimbali ikiwemo ulinzi wamipaka . .
Comments
Post a Comment