SERIKALI YA KUTANA NA WADAU WA MAWASILIANO KUJADILI CHANGAMOTO ZA KIMTANDAO NCHINI .

Tokeo la picha la WIZARA YA MWASILIANO NA UCHUKUZI

Timothy Marko.
KATIKA kukabiliana na changamoto za tehama nchini ,serikali kupitia wizara ya sayansi na teknolojia pamoja nawadau mbalimbali waseketa hiyo wamekutana mapema hii leo jijini Dar es salaam katika kongamano ili kuweza  kujadili masuala mbalimbali ya kimtandao.

Akizungumza na waandishi wa Habari mara baada yakikao hicho jijini Dar es salaam Kaimu Mkurugenzi wa Wizara ya Mawasiliano na Tekinojia Samson Mwera amesema kuwa lengo lamkutano huo nikuweza kuzikutanisha na taaasisi za mawasiliano pamoja na serikali ilikuweza kutoa huduma kwa ufanisi ili kumundolea kero mwananchi pindi atumiapo huduma hizo za mawasiliano .

''Ukilinganisha changamoto za nchi za wenzetu nitofauti na nchi yetu ukiangalia sisi tumekuwa katika matumizi ya kimtandao kama vile huduma yakifedha kupitia simu za kiganjani tofauti nanchi ya uingereza huduma hiyo hawanayo kwahiyo sambamba na ukuwaji wa teknolojia tunakabiiwa na tatizo lakisheria za mitandao na elimu ''Alisema Kaimu Mkurugenzi Samson MWERA .

Mkurugenzi Mwera alisema ushirikiano wa serikali na taasisi za mawasiliano nchini kutaweza kutatua changamoto mbalimbali za kimtandao .

Comments

Popular posts from this blog

Mvua yatatiza mpambano kati ya Simba SC na El Masri

Marubani Wawili Wapoteza Maisha kwa Ajali ya Ndege Zanzibar

Huduma za serikali ya Marekani zakwama kwa mara nyengine