SERIKALI KUSHIRIKIANA NA ASASI ZA KIRAIA KUPATA TAKWIMU SAHIHI.

Tokeo la picha la katibu mkuu wizara ya afya

Katibu Mkuu wa wizara ya Afya Maendeleo ya jamii jinsia wazee na Watoto Dk Uledi ULISIBSYA

Timothy Marko

Serikali kwa kushirikiana na asasi za kiraia leo zimekutana ili kuweza kujadiili mpango wa matumizi na ukusanyaji wa taarifa kupita mifumo ya tehama ilikuweza kuondokana natatizo la upatikanaji wa takwimu zisizo sahihi za ukusanyaji na usambazaji wa taarifa za masuala ya afya .

Akizindua mpango huo jijini Dar es salaam Katibu Mkuu wa wizara ya Afya Maendeleo ya jamii jinsia wazee na Watoto Dk Uledi ulisibsya amesema mpango huo wa ukusanyaji wa takwimu za masuala mbalimbali ya afya kwa njia ya tehama utarahisisha upatikanaji wa takwimu sahihi za masula ya afya ilikuweza kupanga mipango mizuri ya maendeleo .

''Taarifa na takwimu  zinapowekwa kwa mfumo ya kijitali ,taarifa hizo zinakuwa na usahihi ambapo taarifa hizi za kitakwimu zitatuwezesha kuweza kupanga mipango ya maendeleo ya wapi panamahitaji nakwamuda gani huduma hiyo inatakiwa na kwa kiwango gani ''Alisema Katibu Mkuu Dk.Uledi ulisibisya .

Katibu Mkuu Ulisibisya alisema kuwa suala la kupatikana kwa takwimu sahihi unafananishwa na upatikanaji wa dhahabu kwani ukiweza kupata takwimu sahihi utaweza kupanga mipango ya maendeleo .

Alisema kwa kipindi kirefu kumekuwa natatizo lamifumo ya kitakwimu nakufanya baadhi yashughuli za kiserikali kukwama mwaka 2016 kwa kushirikiana nawadau mbalimbali walianzisha mfumo utakaorahisisha upatikanaji takwimu nakuchochea maendeleo nchini .

''tumekubaliana kuwekeza katika takwimu mbaimbali hasa katika mikoa arusha kwa kushirikiana wadau ilikuweza kupata chanjo katika maeneo hayo''aliongeza.



 

Comments

Popular posts from this blog

Mvua yatatiza mpambano kati ya Simba SC na El Masri

Marubani Wawili Wapoteza Maisha kwa Ajali ya Ndege Zanzibar

TANZANIA KUWA MWENYEJI WA CHANGAMOTO ZA MADAWATI YAKIJINSIA JUNE 13