MEYA WA DAR AZITAKA NCHI ZA KIAFRIKA KUJISIMAMIA WENYEWE KATIKA KUTATUA CHANGAMOTO ZA MIUNDOMBINU .

Tokeo la picha la ISAYA MWITA

Meya wa jiji la Dar es salaam Isaya Mwita 

Timothy Marko.
Meya wa jiji la Dar es salaam Isaya Mwita leo amekutana naujumbe wakutoka nchini malawi juu ya kujifunza mradi wa mabasi yaendayo kasi BRT na miradi mbalimbali yamiundo mbinu ili kuweza kudumisha ushirikiano katika sekta hiyo .

Akizungumza na waandishi Meya Issaya mwita amesema kuwa ujio huo wa ujumbe wa kutoka malawi umelenga kukuza miji ya brantaya najiji la Dar es salaam katika miradi mbalimbali ya kimaendeleo ambapo meya huyo alizitaka nchi za afrika kuweza kushirikiana katika miradi yakimaendeleo .

''Hatuna haja ya kujifunza nchi za ulaya wanafanya nini nilazima tujifunze hapa katika bara la afrika kama hivi leo tuepata ugeni kutoka nchini malawi watapata kuona namna yamchanganuo wa bajeti zetu za manispaa ''Alisema ISAYA Mwita .

Mwita alisema badala yakufikiria miji mingine ya nje ya bara lafrika imefanikiwaje nilazima watalamu wanchi za kiafrika kushirikiana nakuweza kutatua changamoto za miundombinu nauboreshwaji wa miji kwa ujumla .

Comments

Popular posts from this blog

Mvua yatatiza mpambano kati ya Simba SC na El Masri

Marubani Wawili Wapoteza Maisha kwa Ajali ya Ndege Zanzibar

Huduma za serikali ya Marekani zakwama kwa mara nyengine