Kitilya wenzake waendelea kusota rumande
- Get link
- X
- Other Apps

UPELELEZI katika kesi inayomkabili Mwenyekiti wa Kampuni inayoshughulikia uwekezaji wa mitaji na dhamana (Egma), Harry Msamire Kitilya na waliokuwa maofisa wa benki ya Stanbic, Shose Mori Sinare na Sioi Graham Solomon bado haujakamilika.
Hayo yamesemwa leo na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Mutalemwa Kishenyi mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Victoria Nongwa.
Kishenyi amedai viongozi wa Mashtaka na Uchunguzi wanafanya jitihada za kukamilisha upelelezi na kwamba muda si mrefu utakamilika.
Wakili wa washtakiwa, Alex Mgongolwa ameutaka upande wa mashtaka kuharakisha upelelezi.
Baada ya kutolewa kwa hoja hizo,Hakimu Nongwa ameahirisha kesi hiyo hadi Februari 16, 2018 kwa ajili ya kutajwa na kuutaka upande wa mashtaka kufanya linalowezekana upelelezi ukamilike.
Awamu ya kwanza ya vielelezo hivyo kutoka nchini Uingereza ilikwisha pokelewa bado wanasubiri awamu ya pili.
|
- Get link
- X
- Other Apps
Comments
Post a Comment