JONAS MKUDE ARUSHA DONGO HILI KWA YANGA,ASEMA KWA KOCHA HUYU MFARANSA MTAKAA,
Mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara
unaanza kesho Jumamosi, lakini upande wa kiungo mkabaji wa Simba, Jonas
Mkude amesema msimu huu ni lazima timu hiyo ichukue ubingwa kutokana na
mambo makubwa ya kiufundi wanayoyapata kutoka kwa viongozi wao wa benchi
la ufundi linaloongozwa na Mfaransa, Pierre Lechantre pamoja na Mrundi,
Masoud Djuma.
Mkude alisema msimu huu Yanga itausikia
mbali ubingwa wa ligi kuu kutokana na mbinu mbalimbali za kiufundi
ambazo makocha hao wamekuwa wakiwapatia kila siku mazoezini.
Alisema mbinu hizo zimewasaidia
kuwajenga kiakili na kistamina, hivyo hivi sasa wanajiamini zaidi
wanapokuwa uwanjani lakini pia kuwa na uwezo wa kutafuta ushindi kwa
njia yoyote ile bila ya kukata tamaa.
“Kwa hiyo msimu huu ni lazima tuchukue
ubingwa wa ligi kuu ili mwakani tuweze kushiriki michuano ya kimataifa,
hatuna njia nyingine ya kutufikisha huko baada ya kutolewa kwenye
michuano ya Kombe la FA.
Comments
Post a Comment