Rugemarila atoa ya moyoni mahakamani..
Na mwandishi wetu, Dar es salaam
JAMES Rugemarila anayekabiliwa na kesi ya utakatishaji fedha leo katika
mahakama ya hakimu mkazi kisutu, amewataja Standard Chartered Tanzania
Ltd na Standard Chartered Hong Kong kuwa ndiyo wezi wa fedha za Escrow.
Wezi hao amewataja mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba baada ya
Mwendesha Mashtaka wa Takukuru, Leornad Swai kueleza upelelezi wa kesi
hiyo haujakamilika, hivyo anaomba iahirishwe hadi tarehe nyingine
"Mwizi ni Standard Chartered Tanzania Ltd na Standard Chartered Hong
Kong ambao wameisababishia serikali hasara ya trilioni 37, pia
nimewapelekea Takukuru washiriki wengine wa fedha hizo, hivyo ninaomba
niendelee kuwa hai ili nije kuwa shahidi mzuri wa upande wa mashtaka
kuhusu wezi hao," amesema. Rugemarila
Pia Rugemarila amedai kuwa wezi hao ndio wamemuibia hata kwenye kampuni anayoisimamia ya VIP ambayo inawadai trillion 16.
Wakili Swai amekiri kuwa ni kweli Rugemarila aliwasilisha taarifa ofisini kwao na wanazifanyia kazi kisha watatoa majibu.
Pia Rugemarila ameiomba mahakama imkubalie akafanyiwe uchunguzi nchini
India kwani anasumbuliwa na ugonjwa wa saratani kwa miaka 9 sasa huku
mshtakiwa mwingine ambaye ni mmiliki wa IPTL Harbinder Singh Sethi
ameiambia Mahakama kuwa tatizo lake la ugonjwa linajulikana.
Kutokana na hatua, Hakimu Simba amesema afya za washtakiwa ni muhimu
hivyo wafanyiwe uchunguzi, pia anautaka upande wa mashtaka ukamilishe
upelelezi kwa wakati, ambapo ameahirisha kesi hiyo hadi January 19,2018
Comments
Post a Comment