Meli inayoteketea baharini katika hatari ya kulipuka na kuzama


Oil tanker on fire
BBC SWAHILI 
Kuna hofu kubwa ya kutokea janga la kimazingira Kusini mwa bahari ya China wakati meli ya kubeba mafuta inazidi kufuja siki mbili baada ya kugongana na meli nyingine ya mizigo.
Maafisa nchini China wamevyambia vyombo vuya habari kuwa meli hiyo iko kweney hatari ya kulipuka na kuzama.
Wakoaji wanaojaribu kufika eneo hilo wanazuiwa na moshi mkubwa.
Wahuhudumu 30 raia wa Irana na 2 wa Bangladesh bado hawajulikani waliko licha ya jitihada za kimataifa kuwaokoa.
Kiwangi cha uchafuzi wa mazingira bado hakijulikani. Chombo hicho bado kilikuwa kinateketea leo Jumatatu.
Licha ya kuwa na usajili wa Panama meli hiyo inamilikiwa na kampuni ya Iran.
Sanchi ilikuwa imebeba tani 136,000 za mafuta ya Iran wakati iligongana na meli ya mizigo ya China Jumamosi usiku.
Wahudumu 21 wa meli ya mizigo cha China waliokolewa.

Comments

Popular posts from this blog

Mvua yatatiza mpambano kati ya Simba SC na El Masri

Marubani Wawili Wapoteza Maisha kwa Ajali ya Ndege Zanzibar

TANZANIA KUWA MWENYEJI WA CHANGAMOTO ZA MADAWATI YAKIJINSIA JUNE 13