MASAUNI ABAINI MADUDU BANDARINI,AUNDA KAMATI .

Tokeo la picha la masauni

Naibu waziri wa mambo ya Ndani ya Nchi Hamad Masauni

Timothy Marko.

Naibu waziri wa mambo ya Ndani ya Nchi Hamad Masauni ameunda kamati yakuchunguza juu ya ubora wa Magari 109 ya Kampuni ya Asholk yaliyoagizwa tangu 2013 na jeshi la polisi kupitia wizara ya mambo ya ndani na kutaka ripoti ya uchunguzi huo kuwasilishwa haraka .

Akizungumza mara baada ya kufanya ukaguzi wa magari hayo katika bandari jijini Dar es salaam Naibu waziri masauni alibaini kuwa magari hayo yenye thamani ya dola milioni 601ambayo nimkopo baadhi ya magari hayo ambayo ni malori yamekuwa hayana viwango nakuweza kukiuka taratibu za uagizwaji bandarini hapo.

''ujwaji wa malori haya yapolisi yanaibua maswali hata ukiangalia mkataba wake unaleta maswali ,kwahiyo nimeamua kuunda kamati yauchunguzi wamagari haya kamati hii itabidi ichunguze msambazaji wa magari haya yote hii nikuhakikisha rasmali za nchini zinatumika ipasavyo ''Alisema Naibu Waziri Hamadi Masauni .

Masauni alitaka kamati zitakazo husika kuweza kushirikiana na Tamesa pamoja Nit ilikuweza kuharakakisha ukaguzi wa magari hayo ilikuweza kutoa ripoti itakayoleta majibu sahihi .

Comments

Popular posts from this blog

Mvua yatatiza mpambano kati ya Simba SC na El Masri

Marubani Wawili Wapoteza Maisha kwa Ajali ya Ndege Zanzibar

TANZANIA KUWA MWENYEJI WA CHANGAMOTO ZA MADAWATI YAKIJINSIA JUNE 13