Kanuni kutozungumza siasa,kufanya biashara katika mabasi yaanza kazi


Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

MAMLAKA ya Usimamizi wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra) imewataka wadau wa usafirishaji wakiwemo wamiliki wa mabasi, madereva na abiria kuzingatia kanuni mpya za leseni ya usafirishaji ikiwemo kutozungumza siasa,dini na kufanya biashara ndani ya basi.
Mkurugenzi wa barabara wa Sumatra Johansen Kahatano akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa barabara za Sumatra, Johansen Kahatono alipokutana na wadau hao kuwapa elimu ya kanuni hizo.

“Nachowataka ni kwamba wadau wa usafirishaji wanatakiwa kuzingatia kanuni hizi kwani zina manufaa kwao,” amesema Kahatano.

Amesema katika kanuni hizo kuna mabadiliko ambayo yamefanyika kwenye leseni za usafirishaji wa mizigo huku zikitengenezwa mpya kwa upande wa usafirishaji wa abairia.
Kahatano amesema kanuni zinawataka abiria kutozungumza masuala ya siasa way a dini ndani ya mabasi wakati wakisafiri.

Ameongeza zitamtaka abiria kuweka wazi mizigo waliyonayo ili iwe rahisi kubaini kama wamebeba mizigo haramu.


Hata hivyo mjumbe wa halmashauri kuu ya Taboa taifa Mwesigwa Kazaula aliomba serikali kuendelea kuboresha mazingira katika sekta hiyo ya usafirishaji kwani ndiyo njia pekee inayowaingizia kipato

Comments

Popular posts from this blog

Mvua yatatiza mpambano kati ya Simba SC na El Masri

Marubani Wawili Wapoteza Maisha kwa Ajali ya Ndege Zanzibar

TANZANIA KUWA MWENYEJI WA CHANGAMOTO ZA MADAWATI YAKIJINSIA JUNE 13