IGP SIRRO AKAGUA MIRADI KINOND0NI

Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP)
Simon Sirro, akimsikiliza OCD wa Wilaya ya Kipolisi ya Magomeni, Salim
Marcuse, wakati alipotembelea moja kati ya miradi ya maendeleo ya Jeshi
hilo inayotekelezwa katika mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni jijini Dar es
salaam.

Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP)
Simon Sirro, akikagua mradi wa maendeleo ya Jeshi hilo unaotekelezwa
katika Wilaya ya Kipolisi ya Magomeni jijini Dar es salaam, mradi ambao
unatarajiwa kuanza kutumika kwa ajili ya kutoa huduma za Kipolisi hivi
karibuni.

Wananchi wa Kigogo Mburahati
jijini Dar es salaam, wakimsikiliza Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Simon
Sirro, ambaye alifika eneo hilo kwa ajili ya kukagua moja kati ya miradi
ya Jeshi la Polisi, ambapo IGP Sirro, aliwataka wananchi hao kuendelea
kushirikiana na Jeshi hilo kwa kuwafichua wahalifu katika maeneo yao.

Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP)
Simon Sirro, akimsikiliza Kamanda wa Polisi mkoa wa Kipolisi wa
Kinondoni Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Muliro Jumanne Muliro,
wakati alipofanya ukaguzi wa miradi ya maendeleo ya Jeshi hilo Mbweni
jijini Dar es salaam katika wilaya ya kipolisi ya Kawe.
Picha na Jeshi la Polisi.
Comments
Post a Comment