Vijana watakiwa kutembelea makumbusho

,
Na stahmil mohamed.
Vijana,wanafunzi wa shule za msingi na sekondari pamoja na vyuo wametakiwa kujijengea tabia ya kutembelea Makumbusho ili kujifunza na kuziendeleza fursa mbalimbali ambazo zilikuwa zinafanywa hapo awali ili kujipatia kipato na kukuza uchumi wa nchi.
 
Hayo yamesemwa na mkurugenzi wa Makumbusho Bw.Audax mabula alipokuwa akizungumza katika maonyesho ya picha ya "Karibu Tanzania"yaliyofanyika  Makumbusho ambapo amewataka vijana kutembelea Makumbusho ambapo wataweza kujifunza vitu mbalimbali kupitia picha ambazo zilipigwa miaka 50
iliyoisha zikionyesha shughuli mbalimbali walizokuwa wakizifanya ambapo hivi Sasa hazitiliwi mkazo hali yakuwa zinafaida kubwa kwa Taifa kiujumla.
Hata hivyo Bw.Mabula ameongeza kwa kusema kuna umuhimu mkubwa kwa vijana wa nchi hii kufatilia mambo yaliyofanywa hapo awali kama kufinyanga,kuchonga na kutengeneza dhana mbali mbali kwa ajili ya kilimo ili kujikwamua kiuchumi hivyo kupitia jumba LA maonyesho LA Makumbusho ya Taifa wataweza kujifunza hivyo vyote pia wataweza kuzijua asili zao kiundani kwani wataweza kujifunza tamaduni za kwao kwa kutumia picha mbalimbali zilizopo hivyo kuna haja kubwa ya kutembelea Makumbusho.
Kwa upande wake balozi wa Denmark ambae alikuwa mgeni rasmi katika onesho hilo LA picha Bw.Einar.H.Jensen amesema kuna haja kubwa ya kujifunza vitu vinavyohusiana na asili zetu kwani vina tija hivyo amewaasa vijana zaidi kutembelea makumbusho kujifunza kwa nadharia kwani wao ndio muhimili mkubwa katika kila Taifa.
Pia kwa upande wa baadhi ya wanafunzi waliohudhuria katika onesho hilo waliotokea shule ya Baobab wamefurahi kushiriki katika onesho hilo kwani wamejifunza vitu vingi ikiwemo kuona namna watu wa zamani walivyokuwa wakijikwamua kiuchumi kupitia shughuli za kilimo,uhunzi na vinginevy

Comments

Popular posts from this blog

Mvua yatatiza mpambano kati ya Simba SC na El Masri

Marubani Wawili Wapoteza Maisha kwa Ajali ya Ndege Zanzibar

Huduma za serikali ya Marekani zakwama kwa mara nyengine