Droo ya Kombe la Dunia 2018 kufanyikaDesemba 1 Urusi


Lionel Messi, the Kremlin and Thomas Muller Droo ya Kombe la Dunia 2018 itafanyika ukumbi wa State Kremlin Palace
Baada ya mataifa 32 kufanikiwa kufuzu fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika mwakani nchini Urusi, droo ya kupanga makundi ya timu hizo itafanyika Ijumaa ya Desemba 1 mjini Moscow.
Kuelekea zoezi hilo baadhi ya Timu ambazo zimepangwa chungu kimoja ni chungu cha kwanza ambacho kina timu mwenyeji Urusi, Ujerumani, Brazil, Ureno, Ajentina, Ubelgiji, Poland na Ufaransa.
Afrika inawakilishwa na Misri, Nigeria, Morocco, Tunisia na Senegal.
Na kuelekea fainali hizo FIFA wamesema mpaka sasa kuna maombi milioni 3.5 ya tiketi na walioomba wengi wao ni wenyeji Urusi.

Vyungu vimepangwa vipi?

Vyungu Kombe la Dunia
Chungu 1 Chungu 2 Chungu 3 Chungu 4
Urusi (wenyeji) Uhispania (8) Denmark (19) Serbia (38)
Ujerumani (1) Peru (10) Iceland (21) Nigeria (41)
Brazil (2) Uswizi (11) Costa Rica (22) Australia (43)
Ureno (3) England (12) Sweden (25) Japan (44)
Argentina (4) Colombia (13) Tunisia (28) Morocco (48)
Ubelgiji (5) Mexico (16) Misri (30) Panama (49)
Poland (6) Uruguay (17) Senegal (32) Korea Kusini (62)

Comments

Popular posts from this blog

Mvua yatatiza mpambano kati ya Simba SC na El Masri

Marubani Wawili Wapoteza Maisha kwa Ajali ya Ndege Zanzibar

Huduma za serikali ya Marekani zakwama kwa mara nyengine