JESHI LA POLISI KUFANYA UCHUNGUZI KUUWAWA KWA ASKARI WAKE.

Image result for lazaro mambosasa
Kamishina kanda Maalum RPC Lazaro  MAMBOSASA
Timothy Marko.
JESHI la POLISI kanda maalumu jijini Dar es salaam limesema linaendelea kufanya uchunguzi wa kuwawa kwa askari wake wakikosi cha kutuliza Ghasia (FFU) Charles senyanga mwenye namba zausajili XG475 huko ukonga jijini Dar es salaam.

Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es salaam Kamishina kanda Maalum RPC Lazaro Mambosasa amesema kuwa tukio hilo lilitokea october 21 majira ya saa sita usiku baada yakushambuliwa nawatu wasiojulikana na kukutwa mwiliwake umelowa damu nakukatwa sikio .

''Jeshi lapolisi lina laani vikali vitendo vya uzalilishaji wa askari wake ikiwemo kufanya uchunguzi wawatuhumiwa waliohusika natukio hilo ''Alisema Kaishina mambo sasa 

Mambo sasa alisema kuwa jeshi hilo linaendelea kufanya uchunguzi katika eneo hilo ambapo uchunguzi wa awali ulioneshakuwa kuna baadhi ya wananchi wasio waminifu wamekuwa wakitoa vitisho katika eneo hilo .
ALISEMA kuwa jeshi hilo litahakisha linawatia nguvuni wote watakao bainika walitenda lakosa hilo watafikishwa mahakamani .
''HAKUNA aliyejuu yasheria nilazima wananchi wote watii sheria asubuhi yaleo nilifanya kikao na feed force unit kuna baadhi ya watu wana vaa sare za polisi lakini sipolisi tutawashugulikia ''Aliongeza 

Comments

Popular posts from this blog

Mvua yatatiza mpambano kati ya Simba SC na El Masri

Marubani Wawili Wapoteza Maisha kwa Ajali ya Ndege Zanzibar

Huduma za serikali ya Marekani zakwama kwa mara nyengine