NECTA YAWATADHALISHA WAMILIKI WASHULE JUU YA VITENDO VYA UDANGANYIFU.
![]() |
Katibu wa Baraza la Mitihani la taifa NECTA Dk.Charles Msonde |
BARAZA la Mtihani la Taifa (Necta) limewataka wasimamizi walimu na watahiniwa pamoja na wamiliki wa shule za Msingi kutojihusisha navitendo vya udanganyifu katika mtihani wa Darasa la Saba unaotarajiwa kuanza kesho .
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Katibu wa Baraza hilo Dk.Charles Msonde amesema kuwa Baraza hilo halitasita kumchukulia hatua mtu yeyote atakayejihusisha na udanganyifu katika mitihani itakayofanyika kwa siku mbili kuanzia tarehe 6na 7 september mwaka huu kwani nikunyume cha sheria za nchi .
''watahiniwa watakao bainika kufanya vitendo vya udanganyifu watafutiwa matokeo yote kwa mujibu wa kanuni za mtihani ninawataka wadau kutoa taarifa katika vyombo husika kila wanapobaini kikundi chochote kinajihusisha navitendo hivyo ''Alisema Dk.Charles Msonde .
Katibu wa Baraza la Mtihani Msonde alisema kuwa katika kipindi cha mwaka huu jumla ya watahiniwa 917,072 wanatarajiwa kufanya mtihani huo kesho ambapo kati yao wavulana 432,744 sawa na asilimia 47.9 wakati wasichana 484,328 wanatarajiwa kufanya mtihani huo kote nchini .
Alisema msomo yatakayo tahiniwa katika mtihani huo nipamoja na kiswahili English SANYANSI ,hisabati na maarifa ya jamii.
Comments
Post a Comment