TANROADS TABORA KUTEKELEZA AGIZO LA JPM UJENZI WA BARABARA ZILIZOBAKI

Na Tiganya Vincent
RS-TABORA
29 AUGUSTI 2017
WAKALA wa Barabara nchini (TANROADS)
mkoani Tabora imesama kuwa tayari imeshaanza kutekeza hatua mbalimbali
za maandalizi ya ujenzi wa barabara ambazo Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli aliagiza ujenzi wake uanze
mara moka wakati akiwa katika ziara ya mkoa huo.
Kauli hiyo ilitolewa jana mjini Tabora na Meneja wa TANROADS Mhandisi Damian Ndabalinze kwenye kikao kazi kiliandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora kwa Mameneja wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mjini Tanzania(TARURA) wa mkoani humo.
Mhandisi Ndabalinze alisema
kuwa katika barabara ya kutoka Kaliua hadi Urambo kazi za awali za kwa
ajili ya kuanza maandalizi ya ujenzi inaendelea katika eneo la mradi.
Alisema kwa upande wa barabara
ya ujenzi wa barabara ya Nyahua hadi Chaya yenye urefu wa Kilometa 84
wameshaanza hatua za awali baada ya Kuwait Fund ambaye ndio watoa fedha
za mkopo wa ujenzi wa barabara hiyo kutokuwa na pingamizi.
Meneja huyo wa TANROADS Mkoa
aliongeza kuwa hivi sasa wanachongojea ni ufunguzi wa zabuni ambayo
itafanyika katika kipindi wiki moja ijayo ili kazi nyingine zianze.
“ Barabara ya Nyahua Chaya
tumepata ‘no objection’ kutoka kwa Kuwait Fund….’consultant’
tulishafungua ile ‘technical’ sasa tunasubiri financial itafunguliwa
tarehe saba Mwezi ujao kwa hiyo tunategemea tukishampata ‘Consultant’
mkataba utasainiwa kwa ajili ya kuanza kazi”alisema Ndabalinze.
Kuhusu tenda kwa ajili ya ujenzi
wa barabara ya Pangale kupitia Kuga hadi Mpanda kwa kiwango cha lami ,
alisema kuwa zimeiva zinatarajiwa kufunguliwa tarehe sita mwezi ujao.
Alisema kuwa ujenzi barabara hiyo kwa kiwango cha lami unatarajiwa kuanza mapema mwakani(2018).
Kwa upande wa barabara kutoka
Ipole mkoani Tabora hadi Rungwe mkoani Mbeya yenye urefu wa kilimeta
172 Mshauri yuko katika eneo la mradi akiendelea shughuli mbalimbali za
michoro na kuchukua vipimo mbalimbali ikiwemo aina ya udongo.
Alisema baada ya Mshauri kukamisha
kazi hiyo itabaki shughuli ya kutafuta fedha kwa ajili ya kuanza
ujenzi wa barabara hiyo kwa kiwango cha lami.
Mwezi uliopita Rais Magufuli
alikuwa na ziara Mkoani Tabora ambapo alimwagiza Waziri, wa Ujenzi ,
Uchukuzi na Mawasiliano kuhakikisha ndani ya Mwezi mmoja Mkandarasi wa
ujenzi wa barabara ya kutoka Kaliua hadi Urambo ambayo ina umbali wa
Kilometa 28 awe katika eneo la tukio.
Barabara nyingine ni ile ya Chaya
hadi Nyahua ambayo ina urefu wa Kilometa 84 alisema ndani ya mwezi moja
na nusu kandarasi iwe imeanza.
Comments
Post a Comment