NIC Bank Yakabidhi Magari Matatu kati ya Sita Kwa Mteja wake kama Mkopo
Meneja
mahusiano kwa wateja wakubwa wa benki ya NIC Tanzania, Woinde
Murro(kulia) akizungumza jambo na mmoja wa wateja waliofika kwaajili ya
kukabidhiwa magari makubwa ikiwa awamu ya kwanza ya mkopo wa Magari Sita
ambapo leo amepokea magari matatu na matela matatu
Meneja mahusiano kwa wateja wakubwa wa benki ya NIC Tanzania, Woinde Murro(kulia) akimkabidhi
funguo Mkurugenzi wa kampuni ya Usafirishaji ya Simera, Bw.Zainul
Dossa(kushoto) za magari matatu waliyokopeshwa na Benki ya NIC
Meneja
Uendeshaji kutoka Kampuni ya Usafirishaji ya Simera, Bw. Arif akiwasha
moja ya gari mara baada ya Benki ya NIC kukopesha magari sita kwenye
kampuni ya Usafirishaji ya Simera leo jijini Dar es Salaam.

Magari matatu kati ya sita yalikabidhiwa na benki ya NIC kama mkopo kwa mteja wao
Leo
benki ya NIC imekabidhi magari makubwa matatu na matela yake kati ya
magari sita ambayo yamekabidhiwa kama mkopo kwa Mteja wao Simera.
Makabidhiano ya Magari hayo yamefanyika katika Ofisi za FAW zilizopo
Barabara ya Nyerere jijini Dar Es Salaam.
Mkurugenzi
wa kampuni ya Usafirishaji ya Simera, Bw.Zainul Dossa amepokea magari
hayo kati ya sita waliyokopeshwa na Benki ya NIC mapema leo huku magari
mengine matatu yatakabidhiwa hivi karibuni.
Comments
Post a Comment