Mkuu wa Samsung Lee Jae-yong afungwa jela miaka mitano juu ya rushwa


Lee Jae-Yong escorted by prison guards in AprilHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Mahakama nchini Korea Kusini imemhukumu bilionea anayetarajiwa kurithi kampuni Samsung Lee Jae-yong kifungo cha miaka mitano jela kwa makosa ya utoaji rushwa.
MTANDAO WA BBC
Bw Lee alikuwa ameshtakiwa kuhusika katika rushwa katika kashfa ambayo pia ilichangia kuondolewa madarakani kwa rais wa zamani wa Korea Kusini.
Kesi hiyo ilikuwa imevutia sana umma huku hasira zikiendelea kupanda dhidi ya kampuni kubwa za kibiashara za Korea Kaskazini, maarufu kama chaebols.
Bw Lee, ambaye amekanusha mashtaka yote, alikuwa amekabiliwa na uwezekano wa kufungwa jela hadi miaka 12.
Bw Lee, ambaye pia hufahamika kama Jay Y Lee na amekuwa ndiye kiongozi wa kampuni hiyo kubwa zaidi ya kuunda simu duniani, amekuwa kizuizini tangu Februari akikabiliwa na tuhuma kadha za rushwa.
Miongoni mwa makosa aliyokabiliwa nayo ni utoaji rushwa, wizi wa mali ya umma na kuficha mali nje ya nchi.
Lee, 49, pia alituhumiwa kutoa mchango wa hisani wa won 41bn ($36m; £29m) kwa nyakfu za hisani zilizosimamiwa na rafiki wa karibu wa rais aliyeondolewa madarakani Park Geun-hye, ndipo apendelewe kisiasa.
Waendesha mashtaka wanasema mchango huo ulitolewa kwa mwandani mkuu wa Bi Park ili serikali iunge mkono mageuzi katika mfumo wa usimamizi wa kampuni ya Samsung ambao ungempatia Lee nguvu zaidi katika udhibiti wa kampuni ya Samsung Electronics.
Wakili wa Lee amesema tayari kwamba watakata rufaa uamuzi huo.
"Tuna imani kwamba hukumu hii itabatilishwa," wakili Song Wu-cheol ameambia wanahabari baada ya kusomwa kwa hukumu, kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters.
Hata hivyo, uamuzi huo wa mahakama ni pigo kubwa kwa kampuni hiyo kubwa zaidi na inayofahamika zaidi ya Korea Kusini.
Image captionPark Geun-hye aliondolewa madarakani Desemba 2016

Comments

Popular posts from this blog

Mvua yatatiza mpambano kati ya Simba SC na El Masri

Marubani Wawili Wapoteza Maisha kwa Ajali ya Ndege Zanzibar

TANZANIA KUWA MWENYEJI WA CHANGAMOTO ZA MADAWATI YAKIJINSIA JUNE 13