MAONESHO YA WAANDISI KUFANYIKA MJINI DODOMA

Image result for PATRICK BALOZI

 Kaimu wa Bodi ya usajili wa Waandisi nchini Muhandisi Patrick Barozi

Timothy Marko.

KATIKA kutathimini mchango wa Waandisi nchini jumuhia ya Waandisi inatarajia kuadhimisha siku ya waandisi september 7 Mwaka huu katika ukumbi wa Jakaya KIKWETE Convetion center uliopo mjini Dodoma .

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es salaam Kaimu wa Bodi ya usajili wa Waandisi nchini Muhandisi Patrick Barozi amesema kuwa maadhimisho hayo yataendana sambamba na kiapo cha watalamu wa uhandisi na maonesho mbalimbali ya kifundi na biashara pamoja nakuwazawadia waandisi wahitimu waliofanya vizuri mitihani ya kuhitimu uhandisi katika kipindi cha mwaka 2016/17.

''Maadhimisho ya mwaka huu yataendana na taasisi mbalimbali kuonesha bidhaa zikiwemo mashine mbalimbali ikiwemo mashine za kushindilia barabara zilizogunduliwa nawatalamu wa kitanzania sambamba na mashine ya kuchakata migomba nakutengeneza nywele za bandia za kinadada ,mashine yakusaga mihogo pamoja namashine za power tiller kwa ajili ya kilimo ''Alisema BAROZI .

Comments

Popular posts from this blog

Mvua yatatiza mpambano kati ya Simba SC na El Masri

Marubani Wawili Wapoteza Maisha kwa Ajali ya Ndege Zanzibar

Huduma za serikali ya Marekani zakwama kwa mara nyengine