Mamia ya watu wazikwa, Sierra Leone
- Get link
- X
- Other Apps
Mtandao wa BBC
Wiizara ya afya
nchini Sierra Leone imesema takriban nusu ya maiti 400 zitokanazo na
maporomoko ya udongo na mafuriko nje ya mji wa Freetown tayari
zimezikwa.
Lakini mkuu wa wataalamu wa magonjwa kutoka mjini Freetown ameiambia BBC kwamba baadhi ya mazishi yalikuwa yamefanyika.
Imefahamika kuwa mazishi hayo yamehusisha miili ambayo tayari ilitambuliwa au ilikuwa imeharibika kabisa.
Watu wapatao mia sita mpaka sasa bado hawajulikani walipo.
Rais wa Sierra Leone ametangaza siku saba za maombolezi.
Nathaniel Williams ni daktari katika hospitali kuu ya Connaught, iliyopo Freetown, anasema hivi sasa kuna tahadhari kubwa ya kutokea magonjwa ya milipuko kama vile kipindupindu
Ameongeza kusema kuwa hivi sasa kunahitajika madawa na vyakula, kwa wale walioathirika.
Hata hivyo, Umoja wa Mataifa nchini humo umesema tayari umeweka mikakati ya kuweza kukabiliana na magonjwa ya milipuko iwapo yatatokea.
Comments
Post a Comment