AfriCOG: Shirika la kutetea haki lavamiwa na maafisa wa serikali Kenya
MTANDAO WA BBC
Polisi na maafisa
wa mamlaka ya mapato nchini Kenya (KRA) leo walifanya jaribio la kuvamia
afisi za shirika moja la kutetea haki ambalo lilikuwa limefutiwa
usajili Jumanne.
Walikuwa kwenye magari wawili wakiwa na agizo walilosema lilitoka kwa mahakama kuwapa idhini ya kufanya uchunguzi katika afizi hizo, wakisema lengo lao lilikuwa kufanya uchunguzi kuhusu tuhuma za ukwepaji kodi.
Maafisa hao hata hivyo walizuiwa kuingia na viongozi wa mashirika ya kutetea haki za kibinadamu.
Wakili Haron Ndubi amesema walitilia shaka uhalali wa agizo la mahakama ambalo maafisa hao walikuwa nalo.
odi ya kusimamia mashirika yasiyo ya kiserikali ilikuwa imetoa agizo la kutaka shirika hilo lifunge ikisema limekuwa likiendesha shughuli zake kinyume cha sheria.
Mkuu wa bodi ya kusimamia mashirika yasiyo ya kiserikali Fazul Mohammed, pamoja na kufutia usajili shirika hilo, alikuwa amependekeza wakurugenzi wake wakamatwe.
Odinga awataka wafuasi wake kususia kazi Kenya
Shirika la AfriCOG liligonga vichwa vya habari mwaka 2013 baada ya kuwasilisha kesi ya kupinga kuchaguliwa kwa Rais Uhuru Kenyatta kwenye uchaguzi uliokuwa umefanyika mwezi Machi.
Taarifa kwenye vyombo vya habari zimekuwa zikidokeza kwamba huenda shirika hilo linapanga kuwasilisha kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi ambayo yalitangazwa Ijumaa ambapo Bw Kenyatta alitangazwa kuwa mshindi.
Umoja wa Mataifa na shirika la Amnesty International wameshutumu hatua ya kuyafunga mashirika hayo mawili na kuitaka serikali kuruhusu mashirika ya kutetea haki pamoja na wanahabari kuruhusiwa kufanya kazi bila kuhangaishwa.
- Uchaguzi Kenya: Ni kwa nini Odinga hataki kwenda kortini?
- Upinzani Kenya wadai Odinga ndiye mshindi wa urais
Amesema ana wasiwasi sana kwamba serikali ya Bw Kenyatta imeanza kuandama mashirika ya kutetea haki za kibinadamu.
Comments
Post a Comment