MAJALIWA AWATAKA WIZARA YA AFYA KUJITATHIMINI .
Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa |
KATIKA kutambua umuhimu wasekta ya afya kwa wananchi wake,serikali imezindua dawati maalum linalohusiana naafya ilikuweza kufanya tathimini ya magonjwa ya mlipuko ilikuweza kudhibiti magonjwa hayo yasiingie katika nchi kupitia mipakani .
Akizindua Mpango huo jijini Dar es salaam Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa amesema mpango huo utaiwezesha serikali na taasisi zake zinazohusiana na masuala ya afya kuweza kutathimini muundo wa uthibiti wamagonjwa ya mlipuko yanayotoka mipakani kupitia dawati la afya .
''Suala la afya ni agenda muhimu kwa nchi zinazoendelea afrika lipo katika hatari zaidi kuingiliwa na magonjwa ya mlipuko kama Ebola uliotokea nchini Congo magonjwa haya hayana mipaka wito wangu mpitie mpango wa dhana hii ''Alisema Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa .
Waziri mkuu Kassimu Majaliwa alisema kuwa magonjwa yamlipuko hajalishi upo upande wazanzibar au upande wa Tanzania bara aliwataka mawaziri wapandezote wa afya kuweza kujadili magojwa ya mlipuko bila kujali mipaka ya majukumu yao kikatiba .
ALISEMA kuwa utekelezaji wampango huo wakudhibiti magonjwa yamlipuko upo katika ilani ya chama chamapinduzi ambapo inalenga watu watakao zalisha mali kuwa na afya bora suala la afya ni agenda ya dunia
Comments
Post a Comment