BoT yazifuta benki tano
Timothy
Marko
Dar
es Salaam. Benki Kuu ya Tanzania(BoT) imezifutia leseni ya kufanya
biashara benki tano na kuziweka chini ya ufilisi.
Taarifa
iliyotolewa leo Alhamisi na BoT imezitaja benki hizo kuwa ni Covenant Bank For
Women (Tanzania) Limited, Efatha Bank Limited, Njombe Community Bank Limited,
Kagera Farmers' Cooperative Bank Limited, na
Meru Community Bank
Limited.
BoT
imeeleza kuwa imefanya hivyo kwa mamlaka iliyopewa chini ya kifungu cha
56(1)(g), 56(2) (a), (b) na (d), 58(2)(i), 11(3)(c) na (j), 61(1) na 41(a) cha
Sheria ya Mabenki na Taasisi za Fedha ya mwaka 2006, Benki Kuu ya Tanzania
imeamua kuzifunga; kusitisha shughuli zake zote za kibenki; kufuta leseni zake
za biashara ya kibenki; na kuziweka chini ya ufilisi.
“Kwa mamlaka
iliyopewa chini ya kifungu Na. 41(a) cha Sheria ya Mabenki na Taasisi za Fedha
ya mwaka 2006; Benki Kuu ya Tanzania imeiteua Bodi ya Bima ya Amana (The
DEPOSIT INSURANCE BOARD) kuwa mfiiisi kuanzia tarehe 04 Januari 2018,” imeeleza
taarifa hiyo.”
“Uamuzi huu
umechukuliwa baada ya Benki Kuu ya Tanzania kujiridhisha kuwa benki hizi zina
upungufu mkubwa wa mtaji kinyume na matakwa ya Sheria ya Mabenki na Taasisi za
Fedha ya mwaka 2006 na kanuni zake. Upungufu huo wa mtaji unahatarisha usalama
wa sekta ya fedha na kwamba kuendelea kutoa huduma za kibenki kwa benki hizo
kunahatarisha usalama wa amana za wateja wake.”
Taarifa hiyo imeeleza
kuwa BoT inapenda kuuhakikishia umma kuwa itaendelea kulinda maslahi ya wenye
amana katika mabenki kwa lengo la kuleta uhimilivu katika sekta ya fedha.
Comments
Post a Comment