Watu wanne wauawa na washukiwa wa al-Shabab Lamu, Kenya

Hindi
Watu wanne wameuawa na watu wanaoshukiwa kuwa wanamgambo wa al-Shabab katika eneo la Hindi katika kaunti ya Lamu katika eneo la pwani nchini Kenya.


MTANDAO WA BBC
Kamishna wa kaunti hiyo Gilbert Kitiyo ameambia BBC kwamba maafisa wakuu wa usalama katika kaunti hiyo wanakutana na watatoa maelezo zaidi baada ya mkutano huo.
Gazeti la kibinafsi la Standard linasema wakazi wamejitokeza barabarani katika mji huo kuandama kulalamikia 'kukawia' kwa maafisa wa usalama kufika eneo la shambulio.
Kisa hicho kimetokea siku chache baada ya watu watatu kuuawa wanamgambo wanaoshukiwa kuwa wanachama wa kundi la al-Shabab waliposhambulia basin a gari eneo la Nyongoro, Witu katika kaunti hiyo ya Lamu.
Gazeti la Standard linasema visa vya mashambulio vimeongezeka eneo hilo wiki za hivi karibuni.
Kamishna wa kanda ya Pwani Nelson Marwa majuzi alitangaza kwamba maafisa wa usalama wangeanza kuangusha mabomu katika msitu wa Boni ambapo wanamgambo wa kundi hilo la Kiislamu wanadaiwa kujificha.
Wakazi waliokuwa wakiishi msituni na karibu na msitu huo walitakiwa kuhama.

Comments

Popular posts from this blog

Mvua yatatiza mpambano kati ya Simba SC na El Masri

Marubani Wawili Wapoteza Maisha kwa Ajali ya Ndege Zanzibar

TANZANIA KUWA MWENYEJI WA CHANGAMOTO ZA MADAWATI YAKIJINSIA JUNE 13