Somalia yaomba Marekani kuisaidia kuwazuia al-shabab kuchimba madini ya Uranium

Serikali ya Somalia
imetuma ombi la msaada wa kijeshi kwa Marekani, kuwazuia wanamgambo wa
al-Shabab kuchimba madini ya uranium ya kuyatuma hadi nchini Iran.
Kwenye
barua waziri wa mashauri ya nchi za kigeni Yusuf Garaad, alisema kuwa
wanamgambo hao wameteka eneo lenye madini ya uranium na wamekuwa
wakichimba madini hayo.Somalia inatajwa kuwa yenye madini ya uranium kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na shirika la kimataifa la kudhibti nishati ya nyuklia
Madai hayo hayajathibitishwa rasmi kuhusu vile uchimbaji huo wa madini ufanywa au ni kwa njia ipi al-Shabab inatuma madini hayo kweda Iran
.
Barua hiyo ilesema kuwa al-Shabab inahusiana na kundi lijulikanalo kama Islamic State wakati limefahamika kuwa na uhusiano wa muda mrefu na al-Qaeda.
Ilisema kuwa tatizo la sasa ni kubwa hata kukishinda kikosi cha Muunganoi wa Afrika kilicho nchini Somalia.
Wizara ya mashauri ya nchi za kigeni haijajibu barua hiyo lakini vyombo vya habari vinasema kwa Marekani ilithibitisha kuipokea barua hiyo.
Comments
Post a Comment