MFUMUKO WABEI WAPUNGUA NCHINI

Mkurugenzi wa sensa ya watu na Takwimu za kiuchumi wa ofisi ya Takwimu nchini Ephraimu Kwesigabo
\
Timoth Marko
MFUMUKO  wa bei nchini  kwamwezi agosti mwaka huu umepungua kwa asilimia 0.4 ikilinganishwa mwezi julai ambapo ulikuwa asilimia 0.2 hali iliyochangiwa nakupungua kwa bei za bidhaa za vyakula .

Thamani ya shilingi umeweza kufikia shilingi92 .20 Kwa mwezi agosti ikilinganishwa na mwezijulai shilingi 91.87

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa sensa ya watu na Takwimu za kiuchumi wa ofisi ya Takwimu nchini Ephraimu Kwesigabo jijini Dar es salaam wakati akizungumza na waandishi wa Habari ambapo amesema kuwa bidhaa za mahindi zimeweza kupungua bei kwa asilimia1.2 ikifuatiwa na unga wamahindi 1.6 huku dagaa ikipungua kwa asilimia 3.4 
 ''Bidhaa kama vile mboga mboga imeweza kupungua bei kwa asilimia 1.2 ikilinganishwa na maharage asilimia 3.2 wakati viazi vikipungua bei kwa 3.5 ''Alisema KWESIGABO 
Kwesigabo alibanisha kuwa wakati bidhaa za mbogamboga ikionesha kupungua bei kwa asilimia 1.2 bei ya pretoli imeonesha kupungua .

Comments

Popular posts from this blog

Mvua yatatiza mpambano kati ya Simba SC na El Masri

Marubani Wawili Wapoteza Maisha kwa Ajali ya Ndege Zanzibar

TANZANIA KUWA MWENYEJI WA CHANGAMOTO ZA MADAWATI YAKIJINSIA JUNE 13