Mashambulizi ya Marekani yawaua al-Shabab 6 Somalia

Jeshi la Marekani limesema kuwa
limewaua wanachama sita wa kundi la wanamgambo wa al-Shabab kwenye
mashambulizi matatu ya angani kusini mwa Somalia.
Oparesheni hiyo ilifanyika kusini mwa Somalia karibu umbali wa kilomita 260 kusini mwa mji mkuu Mogadishu.
Al-Shabab wametangaza kutii kundi la al-Qaeda na wameahidi kutoa mazingira salama kwa mashambulizi ya kigaidi kote duniani
Pia al-shabab wametangazawazi kujitolea katika kupanga na kuendesha mashambulizi dhidi ya Marekani na washirika wake eneo hilo.
Jeshi la Marekani linasema kuwa liitaendelea kutumia kila mbinu kuwalinda raia wake kutokana na vitishi kutoka kwa magaidi kwa lengo na kuwashambulia magaidi na kambi zao za mafunzo kote nchini Somalia na kote duniani.
Comments
Post a Comment