TDB YAWATAHADHARISHA WANANCHI WANAONUNUA MAZIWA KWENYE CHUPA.

Mkurugenzi wa Bodi ya maziwaDkt Mayassa Simba (katikati)
Timoth Marko.

Bodi  ya maziwa nchini (TDB) imewatahadharisha wananchi wote nchini kuepuka kununua maziwa yaliyohifadhiwa kwenye chupa za plastiki na kudai kuwa chupa hizo si salama kwa kuhifadhiwa bidhaa hiyo kwani imekuwa ikitumiwa katika bidhaa zingine na kutupwa mitaani hali inayohatarisha afya za wananchi.

Akizungumza katika mkutano na waandishi jijini Dar Es Salaam mkurugenzi wa masoko wa shirika hilo Mayasa Simba amesema kuwa utumiaji wa maziwa yaliyohifadhiwa kwenye chupa za plastiki haifai kwa matumizi ya kawaida ya binadamu kwani husababisha magonjwa mbalimbali ikiwemo Kifua Kikuu,.

"Soko la maziwa ghafi nchini limetawaliwa na wachuuzi wa maziwa ambao husafirisha maziwa kutoka maeneo ya uzalishaji mijini nas kupata faida  kidogo kutoka na tofauti ya bei ya kununulia na kuuzia, maziwa haya yamekuwa yakihifadhiwa na kuuzwa kwenye chupa za maji ya kunywa za plastiki hivyo kuhatarisha afya ya mlaji|", alisema Mayassa.

Alisema kwa kulitambulia hilo bodi ya maziwa imeanzisha mpango wa ,kituo maalum kitakachokusanya na kuuzia maziwa kwa lengo la kudhibiti ubora na usalama wa maziwa kwa mlaji ili kuondokana na matumizi holela ya uuzwaji wa maziwa kwenye chupa za maji ambazo zimeshatumika.

Comments

Popular posts from this blog

Mvua yatatiza mpambano kati ya Simba SC na El Masri

Marubani Wawili Wapoteza Maisha kwa Ajali ya Ndege Zanzibar

TANZANIA KUWA MWENYEJI WA CHANGAMOTO ZA MADAWATI YAKIJINSIA JUNE 13