TAARIFA KUTOKA JESHI LA POLISI MKOANI MWANZA
TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA KWA VYOMBO
VYA HABARI LEO TAREHE 22.08.2017
- MTU MMOJA AMEUAWA NA KUNDI LA WATU WALIOJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWA KOSA LA WIZI WA KUKU WILAYANI KWIMBA.
KWAMBA TAREHE 21/08/2017 MAJIRA YA
08:45HRS ASUBUHI KATIKA KITONGOJI CHA BUSULWA KATA YA NGULLA WILAYA YA
KWIMBA MKOA WA MWANZA, LEONARD MATHIAS MIAKA 23, MKAZI WA KIJIJI CHA
NGULLA, ALIUAWA NA KUNDI LA WATU WALIOJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWA
KUPIGWA FIMBO NA MAWE SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE KISHA BAADAE
KUCHOMWA MOTO HADI KUPOTEZA MAISHA KWA KOSA LA WIZI WA KUKU WATANO MALI
YA ESTER ROBERT, MKAZI WA KIJIJI CHA NGULLA, KITENDO AMBACHO NI KOSA
KISHERIA.
INASEMEKANA KUWA MAREHEMU ALIIBA KUKU
WATANO NYUMBANI KWA BI ESTER ROBERT KIJIJINI NGULLA KISHA ALIKIMBILIA
KIJIJI CHA JIRANI CHA MWABOMBA. INADAIWA KUWA WANANCHI WA KIJIJI CHA
MWABOMBA WALIPOMUONA MAREHEMU AKIWA NA KUKU HAO WALIPATA MASHAKA KISHA
WALIMKAMATA NA BAADAE WALITOA TAARIFA KIJIJI CHA NGULLA NDIPO MWENYE
KUKU BI ESTER ROBERT ALIFIKA NA KUKABIDHIWA KUKU WAKE .
INADAIWA KUWA BAADA YA MAREHEMU KUKABIDHI
KUKU KWA MWENYE MALI, WANANCHI WALIMCHUKUA NA KWENDA NAE KITUO CHA
POLISI LAKINI WAKIWA NJIANI WALIANZA KUMSHAMBULIA KWA KUMPIGA FIMBO NA
MAWE SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE NA BAADAE KUMCHOMA MOTO. POLISI
WALIPATA TAARIFA KUTOKA KWA RAIA WEMA NDIPO WALIFANYA UFUATILIAJI WA
HARAKA HADI ENEO NA TUKIO NA KUFANIKIWA KUKAMATA WATU SABA AMBAO
WANADAIWA KUHUSIKA KWA NAMNA MOJA AU NYINGINE KATIKA MAUAJI HAYO.
POLISI WAPO KATIKA UPELELEZI NA MAHOJIANO
WATUHUMIWA SABA WALIOKAMATWA, PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA KISHA
IKITHIBITIKA WATUHUMIWA WALIHUSIKA KATIKA MAUAJI HAYO WATAFIKISHWA
MAHAKAMANI. AIDHA UPELELEZI NA MSAKO WA KUWATAFUTA WATU WENGINE
WALIOHUSIKA KWA NAMNA MOJA AU NYINGINE KATIKA MAUAJI HAYO BADO
UNAENDELEA. MWILI WA MAREHEMU TAYARI UMEFANYIWA UCHUNGUZI NA KUKABIDHIWA
KWA NDUGU WA MAREHEMU KWA AJILI YA MAZISHI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU
KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA WAKAZI WA JIJI NA MKOA
WA MWANZA AKIWATAKA KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI NI
KOSA LA JINAI, BALI PINDI WANAPOMKAMATA WAHALIFU AU MHALIFU WAMPELEKE
KWENYE KITUO CHA POLISI ILI HATUA STAHIKI ZA KISHERIA ZIWEZE KUCHUKULIWA
DHIDI YAKE. PIA ANAOMBA WANANCHI WAENDELEE KUTOA USHIRIKIANO KWA JESHI
LA POLISI KWA KUTOA TAARIFA MAPEMA ZA WAHALIFU NA UHALIFU ILI WAWEZE
KUKAMATWA NA KUFIKISHWA KWENYE VYOMBO VYA SHERIA.
IMETOLEWA NA;
DCP: AHMED MSANGI
KAMANDA WA POLISI (M) MWAN
Comments
Post a Comment