Mshindi wa Mzuka Jackpot Akabidhiwa zawadi yake ya Shilingi Milioni 80 jijini Dar es Salaam leo
Balozi
wa Mchezo wa Bahati Nasibu wa Tatu Mzuka, Mussa Hussein (kulia),
akimkabidhi mfano wa hundi ya thamani ya shilingi milioni 80 Mshimdi
Mkuu wa Mchezo huo, Rashid Ally katika hafla iliyofanyika Hoteli ya
Regence Mikocheni Jijini Dar es Salaam leo. Katikati ni Mwakilishi kutoka Baraza la Michezo ya Bahati Nasibu Tanzania, Abdallah Hemed.
Meneja
Masoko wa Kampuni hiyo, Lumuliko Mengele, akizungumza katika hafla
hiyo. Kushoto ni mama wa mshindi huyo, Fatma Kavila. Katikati ni
mshindi, Rashid Ally.
Wapiga picha kutoka vyombo vya habari wakichukua tukio hilo.
Meza
kuu. Kutoka kulia ni Maneja Masoko kutoka Commercial Bank Of Africa
(CBA), Solomon Kawiche. Baba wa mshindi huyo, Kamba Kavila, Meneja
Masoko wa Kampuni ya The Network Product Tatu Mzuka, Lumuliko Mengele,
Rashid Ally na mama yake Fatma Kavila.
Mwakilishi
kutoka Baraza la Michezo ya Bahati Nasibu Tanzania, Abdallah Hemed,
akizungumza katika hafla hiyo ya kumkabidhi mshindi huyo kitita hicho.Rashid Ally akizungumza na wanahabari kuhusu ushindi wake.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Maneja
Masoko kutoka Commercial Bank Of Africa (CBA), Solomon Kawiche,
akizungumza jinsi watakavyomsaidia mshindi huyo jinsi ya kutumia fedha
hizo.
Baba, mama na mwana wakiwa wameshika mfano wa hundi wa kiasi hicho cha fedha alichoshinda mtoto wao.
Na Dotto Mwaibale
MSHINDI
Mkuu wa mchezo wa bahati nasibu ya Tatu Mzuka , Rashid Ally, leo
amekabidhiwa sh.milinoni 80 alizojishindia katika droo kubwa
iliyochezwa Jumapili.
Rashid
ambaye alijishindia kiasi hicho cha fedha katika mchezo huo wa Tatu
Mzuka, alionyesha kutoamini, huku akiwa na furaha na shukrani baada ya
ushindi huo wa kihistoria. Rashid, ambaye ana umri wa miaka 21 tu,
anaishi na familia yake maeneo ya Temeke, Dar es Salaam.
Akizungumzia
ushindi wake, Rashid ambaye amemaliza kidato cha nne hivi karibuni,
alisema kuwa alikuwa anacheza angalau mara 4 hadi 6 kwa wiki kwa kutumia
pesa aliyokuwa anaipata katika shughuli zake za kila siku.
'Ndoto
yangu ni kujenga nyumba, na kuwekeza katika kilimo, kitu ambacho
nitafanya kwa kushirikiana na mama pamoja na Baba yangu. Nia yangu ni
kuikuza iwe ni biashara kubwa ' alisema Rashid.
Pia
alisema ana mpango wa kuendelea kucheza mchezo na kuwa balozi wa Tatu
Mzuka, ili kuwasaidia watu kufurahia mchezo huo na kuuamini.
"Watu
wengine ni wagumu kuamini kwamba unaweza kushinda kiwango hiki kikubwa
cha fedha kupitia shilingi 500 tu. Ninafurahi kuwa miongoni mwa watu wa
kwanza kuthibitisha hili"
Balozi
wa Tatu Mzuka, Mussa Hussein, alisema Tatu Mzuka ina nia ya kuendelea
kutengeneza washindi zaidi wa zawadi ambazo zitabadilisha maisha ya watu
na familia zao.
"Kama
Tatu Mzuka, tunafurahi kuona kwamba mchezo huu unabadilisha maisha ya
Watanzania. Mbali na kiwango kikubwa cha pesa tunachokitoa katika droo
kubwa ya kila Jumapili, tumeishalipa zaidi ya milioni 350 kama ushindi
wa kila siku kwa wachezaji mbalimbali wa mchezo wetu. Kwa wastani mtu
mmoja anakuwa mshindi wa Tatu Mzuka kila sekunde 10, masaa 24 kwa siku,
na siku 7 kwa wiki "alisema Mussa.
Pia
akizungumza katika tukio la kukabidhi ushindi huo, Mwakilishi kutoka
Baraza la Michezo ya Bahati Nasibu Tanzania, Abdallah Hemed alimpongeza
Rashid kwa ushindi huo na akamwomba kuwekeza fedha kwa makini ili
abadilishe maisha ya watu wengine. Hemed aliipongeza Kampuni ya The
Network Product Tatu Mzuka kwa kuendesha mchezo kwa uaminifu na kwa
haki na kutimiza ahadi yake kwa umma.
Comments
Post a Comment