MAKONDA AWATAKA WANANCHI KUHESHIMU MAENEO YALIYOTENGWA KWA MAPUMZIKO.
MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM PAUL MAKONDA |
Mkuu wa mkoawa jiji laDar es salaam Paul Makonda amewataka kwa wakazi wa jiji hilo,kutunza na kulinda mazi ngira ya bustani ya kaburi moja iliyopo
maeneo ya samora katika wilaya ya ilala, katika uzinduzi wa bustani
hiyo ambayo ilijengwa kwa kiasi cha fedha za kimarekani dola 380,000
lengo la eneo hilo ikiwa ni kwa ajili ya wananchi kupumzika.
Makonda
ameyasema hayo leo katika uzinduzi wa eneo hilo, ambapo Mh. Makonda
amekata utepe katika bustani hiyo, ilifanyiwa marekebisho na matengenezo
na wadau wa JAICA, wakiwa na lengo la kuijenga dar es salaam mpya,
ambayo imeleta muonekano mpya na ni faida kwa wananchi wote watakaotumia
sehemu hiyo. Na pia amewataka wafanya biashara wodogo
wadogo(wamachinga) kutokufanya biashara katika eneo hilo.
"Eneo
letu hili siyo la kufanya biashara kwa ndugu zetu (wamachinga) ni eneo
La watanzania wote wanaoitaji kupumzika, tumepajenga ili wananchi wote
hatujajenga ili kufanya biashara la hasha! Hili ni eneo la kupumzika kwa
mtu yeyote anaehitaji kupumzika baada ya kufanya shughuli zao wengine
watapumzika kusubiri magari au mtu anaetaka kujiliwaza anaruhusiwa
kupumzika katika bustani hii" Alisema Makonda.
Hata
ivyo ameongeza kuwa katika kuboresha maeneo yote ya jiji vituo vya
daladala vitafanyiwa marekebisho, ambapo vituo hivyo vikijengwa upya na
kuboresha itakuwa ni sehemu nzuri ya kuweka matangazo,na kumjenga jiji
hilo na lengo la dar es salaam mpya itatimia.
Comments
Post a Comment